Waziri Mkuu wa Japan Kishida na Rais Biden wakutana kabla ya mkutano wa G7 huko Hiroshima huku kukiwa na maandamano, ulinzi unaoimarishwa (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2023
Waziri Mkuu wa Japan Kishida na Rais Biden wakutana kabla ya mkutano wa G7 huko Hiroshima huku kukiwa na maandamano, ulinzi unaoimarishwa
Waandamanaji wakiandamana kupinga mkutano wa Kundi la Nchi Saba (G7) unaoanza leo Ijumaa huko Hiroshima, Japan, Mei 17, 2023. (Xinhua/Zhang Xiaoyu)

HIROSHIMA, Japan – Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida na Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi walikutana Hiroshima kabla ya mkutano mkubwa wa Kundi la Nchi Saba (G7), uliogubikwa na maandamano na hali tete.

Kishida, ambaye anashikilia urais wa zamu wa G7 na atakuwa mwenyeji wa mkutano huo wa viongozi wakuu wa G7 wa siku tatu utakaoanza leo Ijumaa, amefanya mazungumzo na Biden Alhamisi jioni katika mji wa magharibi mwa Japani.

Viongozi hao wawili wamejadili kuimarisha zaidi uwezo wa kujilinda dhidi ya mashambulizi wa muungano wa Japan na Marekani na kuamua kuendeleza ushirikiano kati ya Japan, Marekani na Korea Kusini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo.

Hiroshima, mji ambao uliharibiwa na milipuko ya mabomu ya atomiki ya Marekani Mwaka 1945, umekuwa uwanja wa maandamano makali ya kupinga Kundi la G7 siku chache kabla ya mkutano wake, wakati maafisa wa polisi kutoka nchini kote Japan walionekana wakishika doria mitaani.

Takriban waandamanaji 100 walikusanyika kuanzia siku ya Jumatano hadi Alhamisi mbele ya Jumba la Ukumbusho wa Amani la Hiroshima, linalojulikana pia kama Jumba la Bomu la Atomiki, katika Bustani ya Kumbukumbu ya Amani ya Hiroshima, ambayo itafungwa hadi Jumatatu ijayo kwa sababu ya mkutano huo.

Wakiinua mabango na ishara zenye maandishi kama vile "Ponda Mkutano wa G7" na "Hakuna kufanyika Mkutano wenye mada za Vita," waandamanaji hao walipaza sauti za kauli mbiu kama vile "Hakuna mazungumzo ya viongozi wa Japani na Marekani " na "Ondoa kambi za kijeshi za Marekani nchini Japani."

Waandamanaji hao, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafamilia wa waathirika wa bomu la atomiki, walikusanyika kwenye moja ya barabara kuu huko Hiroshima, iliyokuwa imejaa polisi zaidi ya mara 10 ya idadi ya waandamanaji.

Mwanafunzi wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 anayeitwa Fred ambaye sasa anasoma Lugha ya Kijapani huko Osaka, amesema hakuna kitu cha kutarajiwa kutoka kwenye Mkutano wa G7.

"Mkutano wa viongozi wakuu wa G7 hauna uhusiano wowote na maslahi ya binadamu," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, na kuongeza kuwa ni mchezo kwa kambi hiyo tajiri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha