Karakana ya Lu Ban nchini Ethiopia: "kadi nzuri  ya China ya Elimu ya Ufundi" kwenye Ukanda Mmoja, Njia Moja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 24, 2023
Karakana ya Lu Ban nchini Ethiopia:
Gao Yang akihojiwa na waandishi wa habari. (Picha na Tao Jian/ Tovuti ya Gazeti la Umma)

Mkataba wa ujenzi wa Karakana ya Lu Ban nchini Ethiopia ulitiwa saini mnamo Septemba, Mwaka 2020 na kuzinduliwa rasmi mnamo Aprili, Mwaka 2021. Imejengwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Teknolojia na Elimu cha Tianjin cha China na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Ethiopia.

Mchakato wa kasi na ufanisi hautenganishwi na ushirikiano kati ya shule za China na Ethiopia. Baada ya kutiwa saini, shule ya Ethiopia iliondoa kwa haraka vifaa vya awali vya majaribio, na chini ya hali ya chini ya uzalishaji ilifanya ujenzi wa kiwango cha juu kwa kuendana na michoro ya majengo iliyotolewa na shule ya China.

Gao Yang, ambaye amekuwa akifundisha nchini Ethiopia kwa miaka kumi na kwa sasa ni naibu mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa cha Karakana ya Lu Ban cha Chuo Kikuu cha Teknolojia na Elimu cha Tianjin cha China, amewaambia waandishi wa habari: "Iwe ni shule ya Ethiopia, Wizara ya Elimu ya Ethiopia, au hata Idara ya Forodha ya Ethiopia, wanafanya kila wawezalo kutusaidia katika kusafirisha vifaa vya kufundishia hadi Ethiopia kwa haraka iwezekanavyo. Shule ya China inaratibu kwa haraka walimu, na kuwatumia walimu wa China nchini Ethiopia kutoa mafunzo kupitia mtandao wa intaneti kwa walimu wa huko."

Kwa sababu ya pengo kati ya kiwango cha elimu ya China na Ethiopia, Karakana ya Luban ya Ethiopia inatumia mfumo wa Mradi wa Ubunifu wa Majaribio ya Uhandisi (EPIP, yaani Engineering, Practice, Innovation, Project) kama kielelezo chake cha elimu. Hali hii siyo tu inafundisha wanafunzi ujuzi wa kinadharia, lakini pia hutoa kipaumbele zaidi kwa uendeshaji wa kivitendo. Gao Yang amesema kuwa wanafunzi hao kwa kutumia maarifa waliyojifunza darasani walipokea mradi wa kutengeneza taa za LED na kujipatia kipato. "Walirudi wakikimbia kwa furaha sana, kuinama mara tu walipoingia chumbani, wakasema asante kwa mwalimu, hali ambayo ni muhimu sana!"

Kwa sasa, Karakana ya Luban ya Ethiopia imeshatoa mafunzo kwa zaidi ya wanafunzi 300, wengi wao ambao wameshiriki katika mafunzo muhimu ya ualimu wamehitimu na wamejitolea kwa shughuli za ufundishaji wa wenyeji.

Kuanzishwa kwa Karakana ya Luban kumeipa China kadi yake katika usaidizi wa elimu ya ufundi nchini Ethiopia. Tangu kuanzishwa kwake, imepokea zaidi ya makundi 50 yenye watu zaidi ya 1,000 kutoka Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, na ujumbe wa mawaziri wa Ethiopia kutembelea na kujifunza. Imeanzishwa na Kamati ya Maendeleo ya Rasilimali Watu ya Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kuwa kituo cha utoaji wa ujuzi wa ufundi kwa Afrika nzima na kuhudumia Mradi wa Benki ya Dunia ya Ushirikiano wa Elimu ya Ufundi wa Afrika Mashariki (EASTRIP).

Karakana ya Luban ya Ethiopia imesaidia vijana wenyeji kuboresha ujuzi wao wa kibinafsi, kuboresha kiwango cha jumla cha maendeleo ya elimu ya ufundi ya nchini humo, na kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi na uboreshaji wa maisha ya watu. Ni hatua muhimu ya Ujenzi wa Uwezo katika "miradi minane" ya Ushirikiano kati ya China na Afrika, pia ni mafanikio muhumi katika Ukanda Mmoja, Njia Moja.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha