Teknolojia mpya zilizobuniwa na Kampuni za China zang'aa kwenye maonyesho makubwa duniani ya Wiki ya Vifaa Onyeshi 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 25, 2023
Teknolojia mpya zilizobuniwa na Kampuni za China zang'aa kwenye maonyesho makubwa duniani ya Wiki ya Vifaa Onyeshi 2023
Watu wakitembelea eneo la maonyesho la Kampuni ya Teknolojia ya BOE ya China kwenye maonyesho ya Wiki ya Vifaa Onyeshi 2023 huko Los Angeles, Marekani, Mei 23, 2023. Chapa za China zimepata msukumo mkubwa kwenye Wiki ya Vifaa Onyeshi 2023, ambayo ni maonyesho ya kimataifa ya tasnia ya vifaa onyeshi yanayofanyika wiki hii mjini Los Angeles, Marekani, zikivutia watu wengi na kushinda kutambuliwa kwa teknolojia zao za ubunifu na bidhaa. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)

LOS ANGELES - Chapa za China zimepata msukumo mkubwa kwenye maonyesho ya Wiki ya Vifaa Onyeshi 2023, ambayo ni maonyesho ya kimataifa ya tasnia ya vifaa vya kuonyesha yanayofanyika wiki hii mjini Los Angeles, Marekani, zikivutia watu wengi na kushinda kutambuliwa kwa teknolojia zao za ubunifu na bidhaa.

Maonyesho ya Wiki ya Vifaa Onyeshi 2023, ambayo huandaliwa na Society for Information Display (SID), yamekuwa yakifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Los Angeles kuanzia Mei 21 na yatafikia tamati kesho Ijumaa, Mei 26.

Kuanzia Uhalisia Ulioboreshwa (AR), Uhalisia Pepe (VR), teknolojia ya kiotomatiki, diodi ya kikaboni inayotoa mwanga (OLED), OLED ndogo na vifaa onyeshi vidogo hadi vile vya kuvaliwa, nembo za kidijitali na Karatasi ya Kielektroniki, maonyesho ya Wiki ya Vifaa Onyeshi huwasilisha teknolojia za hivi punde na bora zaidi na maendeleo kutoka kwa tasnia ya kimataifa ya vifaa onyeshi vya kieletroniki na tasnia ya teknolojia ya habari.

Kampuni ya Teknolojia ya BOE, mojawapo ya watengenezaji bidhaa wakubwa duniani katika tasnia ya vifaa onyeshi vya semiconductor na kampuni ya Intaneti ya Vitu (IoT), imeleta teknolojia za hali ya juu kwenye maonyesho hayo, ikijumuisha uzinduzi wa bidhaa mpya chini ya chapa zake za teknolojia za ADS Pro, f-OLED na α-MLED (mini LED), pamoja na programu mpya za kibunifu kama vile uonyeshaji wa akili bandia ndani ya gari, 3D isiyohitaji miwani na metaverse.

Visionox, kampuni ya China ya teknolojia ya hali ya juu yenye teknolojia onyeshi ya OLED, imeleta teknolojia na matumizi ya kibunifu ya vifaa onyeshi kwenye Wiki ya Vifaa Onyeshi, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya kujipanga ya pixelization, kompyuta ndogo zinazobebeka na zinazokunjika, vifaa onyeshi vya matibabu, na vifaa onyeshi vyenye uwazi vya magari.

Eben Yang, Naibu Mkuu wa Visionox, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba Amerika Kaskazini ni moja ya masoko muhimu zaidi ya Visionox nje ya China. Kwa sasa kampuni hiyo inashirikiana na wateja wengi wa Marekani kutoa suluhu za teknolojia onyeshi za vifaa vya Uhalisia Pepe (VR), vifaa vinavyoweza kuvaliwa, simu janja na bidhaa zingine.

"Tunatumai kuchukua fursa za kushiriki katika Wiki ya Vifaa Onyeshi ili kuonyesha teknolojia zetu za kibunifu, kuwapa wateja bidhaa zenye ushindani zaidi, na kupanua zaidi masoko ya ng'ambo," Yang amesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha