Vipepeo wachanga (pupa) karibu milioni 100 wavunja kwa pamoja vifuko vya uzazi kuwa vipepeo kamili huko Yunnan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2023
Vipepeo wachanga (pupa) karibu milioni 100 wavunja kwa pamoja vifuko vya uzazi kuwa vipepeo kamili huko Yunnan, China
Vipepeo wachanga (pupa) wakikusanyika na kukua hadi kuwa vipepeo kamili. Picha imetolewa na Kituo cha vyombo vya habari cha Wilaya ya Jinping.

Kipindi cha mwishoni mwa mwezi Mei, msimu wa kukua kwa vipepeo umeanza kwenye “Bonde la Vipepeo la China la Honghe” katika Kijiji cha Maandi cha Wilaya ya Jinping ya Mkoa wa Yunnan, China. Vipepeo wachanga (pupa) milioni 80 hadi milioni 100 hivi wamevunja vifuko vya uzazi na kukusanyika milimani, hali ambayo imeleta mandhari nzuri ya vipepeo ya kustaajabisha sana.

Katika Kijiji cha Maandi, kuna tofauti kubwa ya miinuko kutoka usawa wa bahari kati ya sehemu mbalimbali, pamoja na eneo kubwa la misitu na kiasi kikubwa cha mvua. Mazingira haya bora ya asili yanasaidia kuzaliana na kukua kwa viumbe mbalimbali, kwa hivyo kimekuwa “Bonde la Vipepeo la China”.

Mkuu wa Makumbusho ya Bonde la Vipepeo katika Wilaya ya Jinping Yang Zhenwen alikadiria kuwa, kilele cha idadi ya vipepeo wanaokua kutoka hatua ya pupa na kuwa vipepeo kamili kitakuwa kati ya tarehe 25 hadi tarehe 31 mwezi wa Mei, na wakati bora wa kuwatazama utaendelea hadi tarehe 25 hivi mwezi wa Juni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha