Baraza la Zhongguancun la Mwaka 2023 lafunguliwa Beijing, likiangazia ushirikiano na uwazi wa kimataifa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2023
Baraza la Zhongguancun la Mwaka 2023 lafunguliwa Beijing, likiangazia ushirikiano na uwazi wa kimataifa
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, akitembelea maonyesho baada ya hafla ya Baraza la Zhongguancun la Mwaka 2023 hapa Beijing, China, Mei 25, 2023. ( Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - Baraza la Zhongguancun la Mwaka 2023 limeanza Alhamisi katika Kituo cha Maonyesho cha Zhongguancun hapa Beijing, China. Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang alihudhuria na kutoa hotuba kwenye ufunguzi wa baraza hilo .

Amesisitiza kuwa, China itaharakisha utekelezaji wa mkakati wa maendeleo yanayotokana na msukumo wa uvumbuzi ili kutoa msaada thabiti kwa maendeleo yenye ubora wa juu ya kiuchumi na kijamii.

"China inapenda kufanya juhudi kubwa za kushiriki katika ushirikiano wa kimataifa wa uvumbuzi, ili kunufaika pamoja na matunda ya maendeleo ya uvumbuzi na dunia nzima," Amesema Ding.

Ametoa pendekezo lenye mambo matatu, akisema kwamba juhudi zinapaswa kufanywa ili kuboresha uongozi wa uvumbuzi wa kimataifa, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya sayansi na teknolojia, na kuimarisha ushirikiano katika utafiti wa masuala ya kimataifa.

"Tunatarajia kushiriki katika mazungumzo ya kina na kuhimiza maelewano na wageni kutoka sekta mbalimbali, kuunganisha hekima ili kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na kutoa mchango kwa ustawi wa uchumi wa Dunia," amesema Wu Zhaohui, Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia wa China.

Zhongguancun ilianzishwa Mwaka 1988 Kaskazini-Magharibi mwa Beijing, ikiwa nyumbani kwa makundi ya vyuo vikuu na taasisi za utafiti. Ni eneo la kwanza la kitaifa la maendeleo ya viwanda la teknolojia ya hali ya juu nchini China na linajulikana kama "Bonde la Silicon la China."

Baraza la Zhongguancun lilianzishwa Mwaka 2007 na limekua na kuwa jukwaa la wazi la ngazi ya kitaifa la uvumbuzi na jukwaa la kimataifa.

Likiwa na kaulimbiu isemayo "Ushirikiano Wazi kwa Mustakabali wa Pamoja wa Baadaye," Baraza hili la mwaka huu limevutia wageni kutoka zaidi ya nchi na kanda 80, pamoja na mashirika ya kimataifa, taasisi na idara za serikali za nchi mbalimbali karibia 200.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha