Kilimo cha Teknolojia za Kidijitali chasaidia wakulima kuongeza kipato huko Guizhou, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2023
Kilimo cha Teknolojia za Kidijitali chasaidia wakulima kuongeza kipato huko Guizhou, China
Mfanyakazi akiangalia halijoto na kiwango cha unyevu ndani ya banda la kuotesha miche katika Kituo cha Kuotesha Mbegu Bora za Mboga cha Nanjiang katika Wilaya ya Kaiyang ya Mji wa Guiyang, Tarehe 23, Mei.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Guizhou kwa kutegemea nguvu bora ya maendeleo ya data kubwa, umehimiza kuharakisha matumizi ya teknolojia za kidijitali katika kilimo cha aina mpya katika umwagiliaji na mabanda ya upandaji wa mimea yanayotumia teknolojia za akili bandia ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa kilimo. Mafungamano ya teknolojia ya kidijitali na kilimo yameleta uhai wa kustawi kwa kilimo cha jadi, na kunawasaidia wakulima kuongeza kipato chao. (Picha zimepigwa na Yang Wenbin/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha