Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Nishani zinazoashiria heshima ya juu zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2023
Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Nishani zinazoashiria heshima ya juu zaidi
Mchana wa Septemba 14, 2022 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China alipokea nishani ya “Tai wa Dhahabu” kutoka kwa Rais Tokayev wa Kazakhstan katika Ikulu ya Nur-Sultan. (Picha na Rao Aimin)

Kuanzia Septemba 14 hadi 16, 2022, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara katika nchi za Asia ya Kati, ambayo ilikuwa ni ziara yake ya kwanza katika nchi za nje tangu kuzuka kwa UVIKO-19. Katika ziara hiyo, Rais Xi alipokea nishani mbili zenye umuhimu mkubwa. Moja ni nishani ya "Tai wa Dhahabu" ambayo ni heshima ya juu zaidi iliyotunukiwa na Kazakhstan. Nyingine ni nishani ya "Urafiki wa Juu Zaidi" iliyotunukiwa na Uzbekistan, ambayo ni nishani ya heshima ya juu zaidi kwa watu wa nchi za nje kutolewa kwa mara ya kwanza na nchi hiyo.

Katika miaka kumi iliyopita, wakati Rais Xi Jinping alipofanya ziara katika Asia ya Kati, alitoa pendekezo la kujenga kwa pamoja "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri" kwa mara ya kwanza nchini Kazakhstan. Katika miaka 10 iliyopita, maendeleo ya Kazakhstan na Uzbekistan yamekuwa kwenye "treni ya mwendo kasi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja". Kituo cha ushirikiano wa usafirishaji mizigo kati ya China na Kazakhstan kilianzishwa huko Lianyungang. Handaki la reli ya "Anglia-Pap" ambalo ni handaki lenye urefu zaidi katika Asia ya Kati lilizinduliwa. Na mabomba manne ya bomba la gesi asilia kati ya China na Asia ya Kati yote yanapita Uzbekistan...

Katika hafla ya kutunukia nishani hiyo, Rais Tokayev wa Kazakhstan alimwambia Rais Xi Jinping: "Umekuwa na uzoefu mkubwa katika kusimamia nchi na una haiba ya kipekee." Rais wa Uzbekistan Mirziyoyev alimwambia Rais Xi Jinping: "Tunaamini kuwa wewe ni mwanasiasa mkubwa na kiongozi mashuhuri zaidi duniani katika zama za hivi leo."

Katika miaka 10 iliyopita, Rais Xi Jinping alifanya ziara mara 42 katika nchi 69 kwenye mabara matano, na ametunukiwa nishani mara nyingi. Kila nishani inaashiria urafiki mkubwa kati ya watu wa China na watu wa nchi mbalimbali duniani, pia ni rekodi ya kuongezeka kwa "makundi ya marafiki" na "mtandao wa wenzi" wa China, ikionyesha kuwa chini ya diplomasia ya kiongozi wa nchi, diplomasia yenye umaalum wa nchi kubwa ya China inaendelea kuanzisha hali mpya ya mambo siku hadi siku katika zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha