Wacheza tenisi ya mezani namba moja duniani wa China Sun na Fan watawazwa mabingwa wa Dunia (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2023
Wacheza tenisi ya mezani namba moja duniani wa China Sun na Fan watawazwa mabingwa wa Dunia
Mshindi wa medali ya dhahabu, Fan Zhendong (wa pili kushoto) wa China, mshindi wa medali ya fedha Wang Chuqin (wa kwanza kushoto) wa China na washindi wa medali ya shaba Ma Long (wa pili kulila) na Liang Jingkun wa China wakishiriki hafla ya kutunuku medali kwa washindi wa fainali za mchezo wa tenesi ya mezani kwa wanaume kwa mchezaji mmoja dhidi ya mmoja ya Mashindano ya Dunia ya Tenisi ya Mezani ya ITTF 2023 huko Durban, Afrika Kusini, Mei 28, 2023. (Xinhua/Han Xu)

DURBAN, Afrika Kusini - Wacheza tenisi ya mezani namba moja kwa ubora duniani wa China Sun Yingsha na Fan Zhendong wameibuka washindi katika fainali za mchezo wa tenesi ya mezani kwa wanaume na wanawake kwa mchezaji mmoja dhidi ya mmoja ya Mashindano ya Dunia ya Tenisi ya Mezani ya ITTF 2023 huko Durban, Afrika Kusini.

Katika fainali iliyowakutanisha wachezaji wote Wachina, Sun alipata mafanikio makubwa kwa kunyanyua kombe lake la kwanza la Ubingwa wa Dunia baada ya kumshinda bingwa wa Olimpiki Chen Meng 4-2, huku Fan akihifadhi taji lake kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Wang Chuqin.

Sun alianguka chini wakati wa kushangilia na kutembea kumkumbatia mchezaji mwenzake ambaye ni mkongwe kwake, kabla ya wawili hao kubeba bendera ya Taifa La China huku wakipokea shangwe za umati wa watu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Durban.

Kwa maana hiyo, China imeshinda taji la mashindano hayo kwa wanawake mmoja dhidi ya mmoja kwa mara ya 15 mfululizo kwenye Mashindano ya Dunia ya Tenisi ya Mezani kuanzia Mwaka 1995.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha