China yatangaza kwa umma wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-16 kwa ajili ya safari ya kwenye kituo cha anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2023
China yatangaza kwa umma wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-16 kwa ajili ya safari ya kwenye kituo cha anga ya juu
Picha hii isiyo na Tarehe ikiwaonyesha wanaanga wa China Jing Haipeng (Kati), Zhu Yangzhu (Kulia) na Gui Haichao ambao watasafiri kwa ajili ya kutekeleza kazi za anga ya juu na chombo cha Shenzhou-16. Wanaanga wa China Jing Haipeng, Zhu Yangzhu, na Gui Haichao watasafiri kwa ajili ya kutekeleza kazi za anga ya juu na Chombo cha Shenzhou-16, na Jing atakuwa kamanda wa ujumbe huo, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limetangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mei 29, 2023. (Xinhua)

JIUQUAN - Wanaanga wa China Jing Haipeng, Zhu Yangzhu, na Gui Haichao watasafiri kwa ajili ya kutekeleza kazi za anga ya juu na Chombo cha Shenzhou-16, na Jing atakuwa kamanda wa ujumbe huo, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limetangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumatatu.

Jing itakuwa mwanaanga wa kwanza wa China kwenda kwenye anga ya juu kwa mara ya nne. Alihusika katika safari ya Chombo cha Shenzhou-7 Mwaka 2008 na kuwa kamanda wa safari ya Chombo cha Shenzhou-9 na Shenzhou-11 Mwaka 2012 na 2016, mtawalia.

Zhu na Gui watakuwa wakifanya safari yao ya kwanza kwenda anga ya juu. Ni wajumbe wa kundi la tatu la wanaanga wa China, ambalo uteuzi wao ulikamilika ilipofika Septemba 2020.

Zhu atafanya kazi kama mhandisi wa chombo katika safari hiyo ya Shenzhou-16. Gui ni profesa kutoka Chuo Kikuu cha Beihang kilichoko Beijing, na atafanya kazi kama mtaalam wa chombo atakayehusika na uendeshaji wa majaribio ya kisayansi katika obiti kwenye chombo katika kituo cha anga ya juu cha China, Tiangong.

Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-16 kitarushwa saa 3:31 asubuhi Jumanne (Saa za Beijing) kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan Kaskazini Magharibi mwa China, amesema Lin Xiqiang, Naibu Mkurugenzi wa CMSA.

Chombo hicho itakuwa safari ya kwanza ya wanaanga baada ya mpango wa kituo cha anga ya juu cha China kuingia hatua ya matumizi na maendeleo.

Wanaanga hao watatu watakaa kwenye obiti kwa takriban miezi mitano, Lin amesema kwenye mkutano huo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha