Hafla ya kuwaaga wanaanga wa China wanaosafiri na Chombo cha Anga ya Juu cha Shenzhou-16 yafanyika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2023
Hafla ya kuwaaga wanaanga wa China wanaosafiri na Chombo cha Anga ya Juu cha Shenzhou-16 yafanyika
Wanaanga wa China Jing Haipeng (Kulia), Zhu Yangzhu (Kati) na Gui Haichao wakishiriki hafla ya kuagwa kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 30, 2023. Hafla ya kuwaaga wanaanga wa China wanaosafiri na Chombo cha Anga ya Juu cha Shenzhou-16 imefanyika leo Jumanne asubuhi katika Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China. (Xinhua/Li Zhipeng)

JIUQUAN - Hafla ya kuwaaga wanaanga wa China wanaosafiri na Chombo cha Anga ya Juu cha Shenzhou-16 imefanyika leo Jumanne asubuhi katika Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China.

Chini ya amri ya Xu Xueqiang, kamanda mkuu wa mpango wa vyombo vya China vinavyobeba binadamu kwenye anga ya juu, wanaanga Jing Haipeng, Zhu Yangzhu na Gui Haichao walianza safari saa 12:44 asubuhi kwa Saa za Beijing.

Hadi kufikia Jumanne ya leo, wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-15 wamekaa katika kituo cha anga ya juu cha China kwa nusu mwaka, na wanajiandaa kuwasili kwa wanaanga hao wa Chombo cha Shenzhou-16.

Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-16 kimerushwa leo Jumanne saa 3:31 asubuhi kwa Saa za Beijing kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha