Wanaanga wa China katika Chombo cha Shenzhou-16 waingia kwenye kituo cha anga ya juu, na watakamilisha makabidhiano ndani ya siku tano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023
Wanaanga wa China katika Chombo cha Shenzhou-16 waingia kwenye kituo cha anga ya juu, na watakamilisha makabidhiano ndani ya siku tano
Picha hii kutoka kwenye skrini iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing Mei 30, 2023 ikionyesha wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-15 na wale wa Chombo cha Shenzhou-16 wakipiga picha ya kundi ndani ya moduli kuu ya Tianhe ya kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Li Jie)

BEIJING - Wanaanga watatu wa China waliosafiri kwenda anga ya juu na chombo cha Shenzhou-16 siku ya Jumanne asubuhi wameingia kwenye kituo cha anga ya juu cha China na kukutana na wanaanga wengine watatu wa China walio kwenye chombo cha Shenzhou-15 siku ya hiyo ya Jumanne, wakianzisha raundi mpya ya mabadilishano ya wanaanga kwenye mzunguko wa obiti.

Wanaanga wa Shenzhou-15 walifungua mlango wa chombo saa 12:22 jioni. (Kwa saa za Beijing). Wanaanga hao watatu walio kwenye kituo cha anga ya juu cha China hadi sasa waliwasalimu wanaanga hao wapya, na wakapiga picha pamoja.

Kukutana kwenye anga ya juu kwa wanaanga hao kumeanzisha raundi ya pili ya mabadilishano ya wanaanga katika obiti katika kituo cha anga ya juu cha China.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China, wanaanga hao sita wataishi na kufanya kazi pamoja kwa siku tano hivi ili kukamilisha kazi zilizopangwa na kazi ya mabadilishano ya wanaanga.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha