Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: "Asante kwa Kondoo na Kuzawadia kwa Chai" yaonesha urafiki mkubwa kati ya China na Mongolia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023
Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi:
Februari 27, 2020, Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na Rais Battulga wa Mongolia wa wakati huo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. (Picha na Liu Bin)

Februari 27, 2020, Rais Battulgawa Mongolia wa wakati huo alikuja China kwa mahsusi akimpa Rais Xi Jinping wa China cheti cha Mongolia kuizawadia China kondoo 30,000. Battulga akiwa kiongozi wa kwanza wa nchi nyingine kufanya ziara nchini China tangu kuzuka kwa UVIKO-19, alisema kuwa watu wa Mongolia wamekuwa na hisia sawasawa na watu wa China wanaokumbwa na janga, na wanapenda kutoa msaada kwa watu wa China katika wakati huo mgumu.

Wananchi wa Mongolia walileta nyama za kondoo zenye ladha nzuri kwa watu wa China wanaopambana kijasiri na janga hilo, wakitumai kuwa watu wa China wataweza kuongeza kinga ya miilini na kuondokana na janga hilo mapema iwezekanavyo.

Kama zawadi ya shukrani, pamoja na vifaa vya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 na mahitaji ya maisha, China pia ilichagua kwa makini majani ya chai yaliyotengenezwa kuwa ya umbo la tofali ya mkoa wa Hubei ambayo chai hiyo inapendwa sana na watu wa Mongolia.

Mwezi Julai 2021, katika mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Mongolia Khurelsukh, Rais Xi alitaja hasa kwamba baada ya kuzuka kwa UVIKO-19, nchi zetu mbili tuliungana mkono kukabiliana na janga hilo, na kulikuwa na simulizi ya kugusa moyo ya "Asante kwa Kondoo na Kuzawadia kwa Chai", ambayo imeimarisha urafiki mkubwa kati ya watu wa nchi zetu mbili.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha