Meya wa Mji wa Moscow, Russia asema majengo katika mji huo yameharibiwa kwa shambulio la droni (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023
Meya wa Mji wa Moscow, Russia asema majengo katika mji huo yameharibiwa kwa shambulio la droni
Picha hii iliyopigwa Mei 30, 2023 ikionyesha jengo lililoharibiwa kwenye eneo la shambulio la droni huko Moscow, Russia, Mei 30, 2023. (Alexander Zemlianichenko Jr/Xinhua)

MOSCOW - Majengo kadhaa yameharibiwa kidogo kwa shambulio la droni mjini Moscow, Russia mapema Jumanne, Shirika la Habari la Russia, RIA Novosti limeripoti, likimnukuu Meya wa Moscow Sergei Sobyanin.

Sobyanin amesema kuwa hakukuwa na ripoti za mara moja kuhusu watu waliopata majeraha makubwa.

Amesema vikosi vyote vya kutoa huduma za dharura vilikuwa katika eneo la tukio, na uchunguzi zaidi kuhusu shambulio hilo unaendelea, amesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha