Rais wa zamani wa Afrika Kusini asema ushirikiano kati ya China na Afrika katika kupunguza umaskini utaleta maisha bora kwa watu wa pande mbili

(CRI Online) Mei 31, 2023
Rais wa zamani wa Afrika Kusini asema ushirikiano kati ya China na Afrika katika kupunguza umaskini utaleta maisha bora kwa watu wa pande mbili

Mkutano wa 12 wa Kongamano la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika umefanyika kuanzia tarehe 30 hadi 31 mwezi Mei mjini Jinhua mkoani Zhejiang, China ukiwa na kaulimbinu ya “Historia ya Miaka 100 ya Ustawishaji na Ushirikiano kati ya China na Afrika”.

Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya video, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Bw. Kgalema Petrus Motlanthe amesema, tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, nchi zinazoendelea siku zote zimekuwa zikitafuta njia ya kutimiza ustawi wa taifa, kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii na kuboresha maslahi ya watu. Lakini kutokana na sababu mbalimbali, juhudi za kupunguza umaskini hazijaleta matokeo sawa katika nchi tofauti.

Amesema China imefanikiwa kutimiza lengo la kutokomeza umaskini uliokithiri, lakini nchi nyingi za Afrika bado zinakabiliwa na shinikizo kubwa la umaskini.

Bw. Motlanthe amesema, mfano wa China umethibitisha kuwa, nchi zinazoendelea zina uwezo wa kuongoza watu wao kuondokana na umaskini na kuboreaha maisha yao.

Amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuondokana na umaskini umeweka msingi imara, pande hizo mbili pia zina nia thabiti ya kisiasa ya kushirikiana kuondoa umaskini, na zimefikia makubaliano muhimu ya kimkakati kwenye nyanja hiyo.

Anaona kuwa, Afrika na China kuimarisha ushirikiano katika kupunguza umaskini, hakika kutaleta maisha bora na yenye heshima kwa watu wa pande zote mbili.

Kongamano la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika, likiwa ni moja ya makongamano muhimu chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), lilianzishwa mwaka 2011 na Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, na limkuwa likihimiza kwa ufanisi mawasiliano na maelewano kati ya China na Afrika. Wajumbe 200 kutoka China na nchi 42 za Afrika wamehudhuria ukumbini au kushirika kwenye kongamano hilo kwa njia ya video.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha