China yajenga mnara wa kihistoria nchini Oman kuashiria urafiki wenye manufaa kwa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 01, 2023
China yajenga mnara wa kihistoria nchini Oman kuashiria urafiki wenye manufaa kwa pande zote
Picha hii iliyopigwa Mei 30, 2023 ikionyesha Mnara wa Zheng He huko Salalah, Oman. (Xinhua/Wang Qiang)

SALALAH, Oman - Ubalozi wa China nchini Oman umeandaa hafla ya kusherehekea kukamilika kwa Mnara wa Makumbusho ya Zheng He katika mji wa pwani wa Salalah katika Jimbo la Dhofar siku ya Jumanne usiku ili kumkumbuka baharia mkuu wa China Zheng He ambaye aliwahi kusafiri kwenye pwani ya Oman pamoja na kuashiria urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili.

Balozi wa China nchini Oman, Li Lingbing, ametoa hotuba kwenye hafla hiyo, na kusema kwamba Oman ni nchi muhimu kando ya Njia ya kale ya Hariri ya Baharini, na mhusika mkuu wa mnara huu, Zheng He, ambaye ni baharia wa China wa Enzi ya Ming (1368-1644), alitembelea Oman, ikiwa ni pamoja na Dhofar, mara nne.

Balozi Li amesema, wakati mwaka huu unatimiza miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, kukamilika kwa Mnara wa Makumbusho ya Zheng He katika wakati huu muhimu wa kihistoria kuna umuhimu maalumu.

Inaaminika kuwa jengo hili la kipekee litakuwa ishara mpya ya kuendelea kwa urafiki kati ya China na Oman katika zama mpya, amesema na kuongeza kuwa litashuhudia kuimarika kwa maelewano na mabadilishano katika nyanja mbalimbali kati ya China na Oman, na kuchangia katika ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja yenye manufaa na maendeleo ya pamoja kwa pande zote mbili, na kuleta manufaa makubwa kwa watu wa nchi zote mbili.

Khalid bin Salim al Saeedi, Mwenyekiti wa Shirikisho la Urafiki kati ya Oman na China, amesema katika hotuba yake kwamba Mnara wa Makumbusho ya Zheng He unaonyesha wazi mabadilishano ya muda mrefu na yasiyokatizwa kati ya ustaarabu wa Oman na China. Viongozi wenye busara wa nchi zote mbili wamejitolea kuendeleza na kukuza uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.

Zheng anatambuliwa sana kama mmoja wa mabaharia waliokamilisha safari nyingi zaidi katika historia ya China. Aliongoza meli kubwa za Enzi ya Ming ya China kufanya safari mara saba katika Asia ya Kusini-Mashariki, Asia ya Kusini, Asia Magharibi, na Afrika Mashariki katika Karne ya 15.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha