Meli ya Doria yenye uzito wa zaidi ya tani elfu kumi yafanya doria ya kwanza kwenye Bandari ya Ghuba ya Beibu ya Bahari ya Kusini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 01, 2023
Meli ya Doria yenye uzito wa zaidi ya tani elfu kumi yafanya doria ya kwanza kwenye Bandari ya Ghuba ya Beibu ya Bahari ya Kusini mwa China
Meli ya doria ya “Doria Baharini 09” ikifanya doria ya kwanza kwenye Bandari ya Ghuba ya Beibu ya Bahari ya Kusini mwa China.

Tarehe 31, Mei, Idara za Usimamizi wa mambo ya bahari za Mikoa ya Guangxi, Guangdong na Hainan ya China zimefanya doria ya kwanza ya mwaka 2023 kwenye Ghuba ya Beibu ya Bahari ya Kusini mwa China, ili kuimarisha ukaguzi na usimamizi wa usalama wa usafiri kwenye ghuba hiyo, na kulinda ujenzi wa njia mpya ya usafiri kwenye nchi kavu na bahari upande wa magharibi wa eneo hilo.

Doria hiyo ilifanyika pamoja na meli kadhaa za doria baharini, zikiwemo meli za “Doria Baharini 09”, “Doria Baharini 1001”n.k. Kati ya meli hizo, meli ya “Doria Baharini 09” ni meli ya doria baharini ya kwanza ya China yenye uzito wa zaidi ya tani elfu kumi, ukubwa wake ni sawa na ukubwa wa viwanja vinane vya mpira wa kikapu, na ikijazwa mafuta ya kutosha inaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita zaidi ya 18,000 bila kuongezwa mafuta.

Doria hii imehusisha kukagua maeneo ya bandari kuu kando ya Ghuba ya Beibu, njia za usafiri kwenye bahari, njia za usafirishaji bidhaa na eneo la mpaka kati ya China na Vietnam, ikichukua umbali wa jumla wa zaidi ya maili 430.

Chen Zhongming, naibu kamanda wa doria hiyo ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa Kituo cha Kamandi cha Idara ya Usimamizi wa mambo ya bahari ya Guangxi ameeleza kuwa, doria hiyo imeweka mkazo katika ukaguzi wa mazingira ya usafiri, utaratibu wa usafiri na mazingira ya maji ya Ghuba ya Beibu.

Picha zimepigwa na Zhang Fang, Mo Weihua na Xu Biyuan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha