Kenya yafanya mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu maparachichi kwa ajili ya kupanua soko la China

(CRI Online) Juni 01, 2023
Kenya yafanya mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu maparachichi kwa ajili ya kupanua soko la China
Muonyeshaji wa maparachichi akisubiri watembeleaji wa maonyesho kwenye Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Parachichi wa Afrika (Avocado Africa 2023) jijini Nairobi, Kenya, Mei 31, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu maparachichi ya Afrika umefanyika mjini Nairobi, ambapo maofisa waandamizi, wadau na wakulima wa maparachichi wameeleza matumaini yao ya kuongeza mauzo ya maparachichi kwa China.

Mkuu wa idara ya maendeleo ya mazao katika wizara ya kilimo ya Kenya Bw. Phillip Kello Harsama amesema kuongeza mauzo ya maparachichi kwa China, kutakuwa muhimu katika kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa Kenya.

Amesema watawahamasisha wakulima wengi wa Kenya kupanda maparachichi aina ya Hass yanayoagizwa na China.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa afya ya mimea ya Kenya Bw. Theophilus Mutui, amesema serikali ya Kenya imetoa kipaumbele kwa utekelezaji wa hatua za karantini ili kuhimiza uuzaji wa maparachichi kwenye masoko mapya ikiwa ni pamoja na China.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha