Wanadiplomasia na madaktari wa China watembelea kituo cha watoto yatima nchini Algeria kabla ya siku ya kimataifa ya watoto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 01, 2023
Wanadiplomasia na madaktari wa China watembelea kituo cha watoto yatima nchini Algeria kabla ya siku ya kimataifa ya watoto
Balozi wa China nchini Algeria Li Jian (kushoto) akimkabidhi msaada Sofiane Guercif, Mkurugenzi wa Kijiji cha Watoto cha Draria huko Algiers, Algeria, Mei 31, 2023. Kituo hicho cha watoto yatima Jumatano kilikaribisha hafla ya hisani iliyoandaliwa na ubalozi wa China kuelekea Siku ya Kimataifa ya Watoto inayoadhimishwa leo Juni 1. (Xinhua)

ALGIERS – Kijiji cha Watoto Yatima cha Hilali Nyekundu cha Draria huko Algiers, Algeria, Jumatano kilikaribisha hafla ya hisani iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini humo kuelekea Siku ya Kimataifa ya Watoto ambayo inaadhimisha leo Juni 1 kote duniani.

Kwenye hafla hiyo, madaktari wa timu ya matibabu ya China nchini Algeria waliongea na watu na kuwafundisha mambo ya afya kwenye eneo husika kwa ajili ya watoto wanaoishi katika kijiji hicho.

Michezo na shughuli mbalimbali ziliandaliwa na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la Serikali ya China (CSCEC) Tawi la Algeria, na zawadi, vifaa vya huduma ya afya, na vifaa vya masomo vyenye thamani ya dinari milioni 2 za Algeria (kama dola 14,617 za Kimarekani) vilitolewa kwa watoto.

“Ni mwaka wa saba mfululizo kwa CSCEC Algeria kuchangia Kijiji cha Watoto cha Draria,” amesema Mwenyekiti wa CSCEC Algeria Tang Hao.

Balozi wa China nchini Algeria Li Jian alisema katika shughuli hiyo kwamba China ni "rafiki wa kudumu na mshirika wa dhati wa Algeria, akitumai kuwa urafiki wa China na Algeria utarithishwa kizazi hadi kizazi."

Ameeleza matumaini yake kwamba "watoto watakuwa na wakati maalum na wa furaha katika Siku ya Kimataifa ya Watoto," na amewatakia ukuaji wenye afya na mafanikio katika masomo yajayo.

Sofiane Guercif, mkurugenzi wa kijiji hicho cha watoto yatima, amesema shughuli hiyo imeonesha vilivyo "urafiki kati ya watu wa Algeria na China," akiongeza kuwa vifaa na zawadi zinazohitajika zimewafanya watoto kuhisi ukarimu na utu wema kutoka China.

Kijiji cha Watoto cha Draria ni shirika la hisani lenye makao yake makuu mjini Algiers ambalo hutoa msaada wa kimataifa kwa watoto yatima. Kwa sasa linasaidia watoto 72 wenye umti kati ya miaka 4 na 22. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha