Wataalamu wa mchele chotara kutoka China waisaidia Madagascar kufikia usalama wa chakula

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 01, 2023
Wataalamu wa mchele chotara kutoka China waisaidia Madagascar kufikia usalama wa chakula
Hu Yuefang (wa pili kushoto), mtaalamu wa mchele chotara kutoka China, akifanya kazi na wakulima wa eneo hilo katika shamba la Mahitsy, mji ulioko umbali wa kilomita 35 Kaskazini-Magharibi mwa Antananarivo, Madagascar, Mei 12, 2023. (Xinhua/Sitraka Rajaonarison)

ANTANANARIVO – Katika Madagascar, nchi ya kisiwa cha Bahari ya Hindi, mwezi wa Mei ni msimu wa vuli. Hu Yuefang, mtaalam wa mpunga chotara kutoka China, anakimbia na muda kuvuna mpunga chotara kwenye kipande cha mwisho cha ardhi pamoja na wakulima wenyeji katika shamba lililoko kituo kidogo cha Afrika cha Kituo cha Utafiti na Maendeleo cha Mpunga cha China huko Mahitsy, mji ulioko umbali wa kilomita 35 Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.

"Kumekuwa na mvua nyingi, na hali ya joto imekuwa chini sana katika siku chache zilizopita, kwa hivyo uvunaji unapaswa kufanywa haraka," mtaalamu huyo wa China mwenye umri wa miaka 65 anasema.

Ulimaji wa mpunga ndiyo shughuli kuu ya kilimo nchini Madagascar. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zaidi ya nusu ya mashamba yote yametengwa kwa ajili ya kilimo cha mpunga, na zaidi ya theluthi mbili ya kaya za Madagascar zinalima mpunga. Hata hivyo, kutokana na mambo kadhaa, kama vile ubora wa mbegu, mbinu za kilimo na miundombinu, uzalishaji wa mpunga nchini humo hauwezi kukidhi kikamilifu mahitaji ya chakula ya wakazi wake, na kuilazimu nchi hiyo kukimbilia kuagiza chakula kutoka nje.

Kuanzishwa kwa mpunga chotara wenye mavuno mengi kwa kila eneo linalolimwa kumeipa Madagascar matumaini ya kuweza kujitosheleza kwa chakula. Tangu Mwaka 2007, nchi hiyo imekuwa ikishirikiana na China katika ulimaji na ukuzaji wa mpunga chotara.

Mwaka 2008, Hu Yuefang aliondoka katika mji aliozaliwa wa Yiyang, katika Jimbo la Hunan, Kusini mwa China na kwenda katika kisiwa hicho cha Afrika akiwa mtaalamu wa ulimaji wa mpunga chotara. Tangu wakati huo, amekuwa akitafiti ili kuzifahamu aina za mchele chotara unaoendana na hali ya asili ya eneo hilo na kusaidia wenyeji kutafuta njia bora ya kuongeza uzalishaji wao.

Mara tu baada ya kuwasili, Hu aligundua kwamba mazingira ya asili hapa yalikuwa tofauti sana na yale ya China, na kwamba haiwezi kutumia moja kwa moja uzoefu wa utafiti uliofanywa katika nchi yake mwenyewe.

Mwaka 2010, Hu na timu yake walifanikiwa kuchagua aina tatu za mpunga chotara zenye uwezo wa kupata mavuno mengi katika maeneo ya chini, ya kati na ya juu, na kupokea uthibitisho wa kiufundi kutoka kwa Wizara ya Kilimo ya Madagascar ili kukuzwa na kupandwa kote nchini humo.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, pamoja na kutoa mafunzo kwa mamia ya wataalam na wakulima wenyeji, Hu amekuwa akipatikana wakati wote ili kutoa ushauri mwingi wa kiufundi.

Kutokana na juhudi za pamoja za Hu na wataalam wengine wa China, eneo la jumla la kilimo cha mpunga chotara wa China nchini Madagascar limezidi hekta 50,000, na mavuno ya wastani ya karibu tani 7.5 kwa hekta. Madagascar imepiga hatua kubwa kuelekea kujitosheleza kwa chakula.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha