Macao yaandaa Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji na Ujenzi wa Miundombinu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2023
Macao yaandaa Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji na Ujenzi wa Miundombinu
Mtu akitembea kulipita eneo la maonyesho la Shirika la Ujenzi wa Nishati la China wakati wa Kongamano la 14 la Kimataifa la Uwekezaji na Ujenzi wa Miundombinu huko Macao, Kusini mwa China, Juni 1, 2023. (Xinhua/Cheong Kam Ka)

MACAO - Kongamano la 14 la Kimataifa la Uwekezaji na Ujenzi wa Miundombinu limefunguliwa Alhamisi katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao nchini China, likionyesha maendeleo ya kijani katika sekta hiyo na kujadili mbinu mpya za maendeleo endelevu.

Likiwa na kaulimbiu isemayo "uongozi wa kijani, teknolojia za kidijitali za akili bandia, uwezeshaji wa kifedha, ushirikiano wa kunufaishana," kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili limevutia zaidi ya watu 3,000 kutoka zaidi ya nchi na maeneo 60, wakiwemo zaidi ya maafisa 40 wa ngazi ya mawaziri na watendaji wakuu wa taasisi za fedha.

Kongamano hilo pia limeandaa maonyesho maalum, yakilenga muunganisho wa kikanda, utoaji wa hewa chache ya kaboni na teknolojia za kidijitali za akili bandia.

Ding Yanzhang, mwenyekiti wa Shirika la Ujenzi wa Umeme la China, ambalo ni kampuni jumuishi ambayo hufanya uwekezaji na ujenzi wa miradi ya nishati safi na inayotoa hewa chache ya kaboni na miundombinu, amesema kampuni yake itatoa ufumbuzi mbalimbali na wa jumla wa ujenzi wa miundombinu katika suala la nishati za kisasa, miji ya kisasa na uchimbaji madini wa kisasa.

"Pia tuko tayari kufanya kazi na washirika kutoka kote duniani," Ding amesema, akiongeza kuwa kampuni hiyo ilikuwa imefanya miradi 110 katika nchi 29.

Hu Guodan, mwenyekiti wa Kampuni ya China ya Urban and Rural amesema kampuni yake itaendelea kuongeza uwekezaji katika utafiti na maendeleo ya teknolojia zinazotoa hewa chache ya kaboni katika masuala ya maji na kuhimiza maendeleo ya teknolojia kupitia ushirikiano wa kimataifa.

Kongamano hilo linachukuliwa kama jukwaa la tasnia ya miundombinu ya kimataifa kutafuta fursa za ushirikiano katika maendeleo endelevu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha