Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-15 wawasili Beijing baada ya kutoka Anga ya Juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2023
Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-15 wawasili Beijing baada ya kutoka Anga ya Juu
Mwanaanga wa China Zhang Lu akipokea shada la maua kutoka kwa mke wake baada ya kuwasili Beijing, China, Juni 4, 2023. Wanaanga watatu wa China kutoka chombo cha Shenzhou-15 cha China cha kubeba binadamu kwenye anga ya juu wamewasili Beijing kwa ndege siku ya Jumapili baada ya kurejea salama Duniani kufuatia safari ya miezi sita kwenye kituo cha anga ya juu cha China. (Xinhua/Li Jie)

BEIJING - Wanaanga watatu wa China kutoka chombo cha China cha kubeba binadamu kwenye anga ya juu cha Shenzhou-15 wamewasili Beijing kwa ndege siku ya Jumapili baada ya kurejea salama Duniani kufuatia safari ya miezi sita kwenye kituo cha anga ya juu cha China.

Wanaanga hao wataingia katika kipindi cha karantini ya kimatibabu na kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kimatibabu na tathmini za kiafya, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China.

Watakutana na waandishi wa habari mjini Beijing baada ya kupumzika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha