Ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika wastawi kutokana na uhusiano wa karibu kati ya watu wa pande mbili (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2023
Ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika wastawi kutokana na uhusiano wa karibu kati ya watu wa pande mbili
Picha hii iliyopigwa Tarehe 23 Mei 2023 ikionyesha treni za Reli ya Mombasa-Nairobi jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Wang Guansen)

Ili kuadhimisha Siku ya Watoto ya Kimataifa ya mwaka huu ambayo iliadhimishwa Alhamisi iliyopita, China na Shirika la Wake wa Marais wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD) walizindua kwa pamoja kampeni ya "Kufurahisha Mioyo ya Watoto, Hatua ya Pamoja kati ya China na Afrika" ili kuamsha uelewa wa umma na kuonyesha upendo na kujali kwake kwa watoto wa Afrika.

Kampeni hiyo iliyoanzishwa na Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, na Shirika la Wake wa Marais wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD), ilizinduliwa katika makumi ya nchi za Afrika hivi karibuni.

Katika kipindi cha miongo sita iliyopita, China na Afrika, zikiwa na uhusiano wa karibu kati ya watu wake, zimefurahia ushirikiano unaozidi kuongezeka wa kunufaishana.

Katika mkoa wa Qinghai, Kaskazini Magharibi mwa China, watoto wengi wana hisia maalumu kwa Jamhuri ya Kongo. Mnamo Aprili 2010, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha Richta 7.1 lilitokea katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watibet ya Yushu huko Qinghai. Huku wenyeji wakihangaika kujenga upya nyumba zao, Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso alitangaza kuwa nchi yake itasaidia kujenga upya shule ya msingi katika eneo lililokumbwa na tetemeko hilo. Miaka miwili baadaye, ujenzi upya wa Shule Kuu ya Bweni ya Wenle ulikamilika chini ya jina jipya la Shule ya Msingi ya Urafiki wa China na Kongo.

Judith Vandsla Peter, ambaye anasimamia kudumisha mfumo wa ishara wa reli ya Standard Gauge ya Mombasa-Nairobi, anasema kuwa hatasahau wakati aliotumia na "mwalimu wake wa China" katika miaka minne iliyopita.

Baada ya mafunzo na vitendo, Judith ana uwezo wa kutosha wa kushughulika na kazi yake na atachukua kazi ya ukarabati kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa China. "Watakaporudi China, nitawakumbuka," anasema.

Tangu reli hiyo ianze kutumika 2017, imesafirisha zaidi ya abiria milioni 10 na zaidi ya tani milioni 25 za mizigo, hali ambayo imesukuma maendeleo ya kiuchumi ya maeneo yaliyo karibu na reli hiyo nchini Kenya.

Mnamo Aprili 1955, Mkutano wa Bandung ulifanyika nchini Indonesia, ambapo viongozi wa China na Afrika walipeana mikono, ikiashiria mwanzo wa mawasiliano ya kirafiki kati ya pande hizo mbili.

Mwaka 2013, China ilitoa kanuni za udhati, matokeo halisi, urafiki na nia njema na kutafuta maslahi makubwa zaidi na ya pamoja, ili kuongoza ushirikiano wake na Afrika.

Tangu Machi 2013 baada ya Xi Jinping kuchaguliwa kuwa Rais wa China , Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefanyika mara mbili, na pande hizo mbili zimekuwa zikifanya juhudi katika kuendeleza mipango 10 ya ushirikiano, mapendekezo makuu 8 na miradi 9.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, marais watatu wa nchi za Afrika wamefanya ziara nchini China. Rais wa Eritrea Isaias Afwerki alisema katika ziara yake mjini Beijing mwezi uliopita kwamba mageuzi ya utaratibu wa kimataifa yako katika hatua muhimu na nchi za Afrika bado zinakabiliwa na umwamba na kutotendewa kusiko na haki na usawa.

Jumuiya ya kimataifa inatarajia na inaamini kuwa China itatoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo na upigaji hatua wa binadamu na kwenye haki na usawa wa kimataifa, Afwerki alisema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha