

Lugha Nyingine
Jamhuri ya Watu wa China yafungua rasmi ubalozi katika Jamhuri ya Honduras (4)
![]() |
Yu Bo (wa pili kushoto, mbele), Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Honduras, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Eduardo Reina (wa tatu kushoto, mbele) wakishiriki kwenye hafla ya kufunguliwa rasmi kwa ubalozi wa China huko Tegucigalpa, Honduras, Juni 5, 2023. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua) |
TEGUCIGALPA - Jamhuri ya Watu wa China imefungua rasmi ubalozi wake katika Jamhuri ya Honduras siku ya Jumatatu, kufuatia kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili Machi 26 mwaka huu.
Yu Bo, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Honduras, amesema katika hafla ya kufunguliwa kwa ubalozi kwamba, Honduras imechukua fursa ya kihistoria kufanya uamuzi muhimu wa kutambua kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Amesema, kwa uamuzi huu, Honduras imekuwa nchi ya 182 kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China, uamuzi ambao China inathamini sana.
"Kanuni ya kuwepo kwa China moja ni makubaliano ya kila upande ya jumuiya ya kimataifa na kanuni inayotambuliwa kwa mapana katika uhusiano wa kimataifa," amesema.
Katika muda usiofikia miezi mitatu baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Honduras, nchi hizo mbili zimeongeza kwa haraka uratibu na ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara, kilimo, sayansi na teknolojia, utamaduni, elimu na vyombo vya habari.
Ubalozi wa China nchini Honduras utafanya iwezavyo kutimiza wajibu wa kuwa dirisha linalofungua uhusiano kati ya nchi hizo mbili, daraja linaloimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili na kiungo kinachounganisha watu wa pande hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras, Eduardo Reina, ambaye kwa pamoja amefungua ubalozi huo, amepongeza kufunguliwa rasmi kwa ubalozi wa China na kusisitiza kuwa uamuzi wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China ni chaguo la kujiamulia lililofanywa na Honduras.
Amesema uamuzi huo unapanua uhusiano wa kimataifa wa Honduras na kuendana na nchi nyingi zinazotambua kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Ikifuata kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja, Honduras inatarajia kuhimiza kwa pamoja ushirikiano wa kibiashara na China ili kuboresha miundombinu, kuchangia manufaa kwa watu wa Honduras na kuharakisha ustawi wa kijamii, amesema Reina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma