Rais Xi Jinping ahimiza juhudi endelevu za kukabiliana na kuenea kwa hali ya jangwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2023
Rais Xi Jinping ahimiza juhudi endelevu za kukabiliana na kuenea kwa hali ya jangwa
Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiongoza kongamano la kuimarisha kinga na udhibiti wa pande zote dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa na kuhimiza ujenzi wa miradi muhimu ya ikolojia, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Misitu ya Sanbei (maeneo matatu ya China ya Kaskazini Magharibi, Kaskazini na Kaskazini Mashariki), na kutoa hotuba muhimu huko Bayannur, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China, Juni 6, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

BAYANNUR, Mongolia ya Ndani – Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa wito wa kuendelea na juhudi za kufanya miujiza mipya katika kukabiliana na kuenea kwa hali ya jangwa.

Rais Xi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi kuanzia Jumatatu hadi Jumanne katika mji wa Bayannur, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China.

Ziwa la Wuliangsu ni eneo kubwa zaidi la ardhi oevu la ziwa katika eneo la mtiririko wa Mto Manjano, na ni mazingira ya asili yanayozuia vyanzo vya dhoruba za mchanga zinazoathiri Beijing na Tianjin. Kwenye ziara yake katika eneo hilo la ziwa Jumatatu alasiri, Rais Xi ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kulihudumia na kulilinda kwa kufuata njia safi ya kusonga mbele ili kuwawezesha watu wa vizazi vijavyo kuishi katika nchi nzuri ya China yenye milima mirefu, ziwa lenye maji safi na mazingira yenye hewa safi.

“Mifumo ya kiikolojia ya Kaskazini-Mashariki mwa China, Kaskazini mwa China, na Kaskazini-Magharibi mwa China ni yenye hali dhaifu, na kufanya mapambano dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa kuwa kazi ya muda mrefu,” amesema Rais Xi, huku akihimiza jitihada hizo kuendelea katika eneo la misitu la kitaifa la Linhe.

Baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya miradi ya kimkakati, Jumanne alasiri, Rais Xi aliongoza kongamano katika mji wa Bayannur kuhusu kuimarisha kinga na udhibiti wa pande zote dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa na kuhimiza ujenzi wa miradi muhimu ya ikolojia, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Misitu ya Sanbei (maeneo matatu ya China ya Kaskazini Magharibi, Kaskazini na Kaskazini Mashariki) ya Ulinzi wa Ikolojia (TSFP).

Rais Xi amesema katika hotuba yake kwenye kongamano hilo kwamba, baada ya kufanya juhudi zisizolegalega katika miaka zaidi ya 40 iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika kuzuia na kudhibiti kuenea kwa hali ya jangwa, na kufikia mageuzi ya kihistoria kutoka "mchanga unaolazimisha wanadamu kurudi nyuma" hadi "miti inayolazimisha mchanga kurudi nyuma" katika maeneo muhimu.

Maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja na mtazamo wa kiikolojia wa maeneo ya jangwa, yamepitia mabadiliko makubwa sana, Rais Xi amesema, huku akiongeza kuwa hatari za dhoruba za mchanga na mmomonyoko wa udongo zimedhibitiwa ipasavyo.

Amesema, China inapaswa kutumia fikra za mifumo na kuanza kuwa na mtazamo kamili wa kuboresha mifumo ya ikolojia yake kwa kuhimiza uhifadhi jumuishi na urejeshaji wa mazingira ya asili ya milima, maji, misitu, mashamba, maziwa, mbuga na majangwa.

Rais Xi amesisitiza kupigana vita dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa katika maeneo matatu muhimu. Kwa Jangwa la Mu Us, Jangwa la Kubuqi, na Mlima Helan, juhudi zitafanywa kurejesha mazingira ya asili ya mito, maziwa, ardhi oevu, na mbuga ili kuongeza uwezo wa eneo hilo katika kuzuia mchanga na ulinzi wa maji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha