Gazeti la People's Daily na vyombo vya habari vya Laos waanza kampeni ya mahojiano ya pamoja kuhusu ushirikiano wa BRI huko Vientiane (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2023
Gazeti la People's Daily na vyombo vya habari vya Laos waanza kampeni ya mahojiano ya pamoja kuhusu ushirikiano wa BRI huko Vientiane
Waandishi wa habari kutoka gazeti la People's Daily la China na vyombo vya habari vya Laos wakifanya mahojiano ya pamoja katika Eneo la Saysettha la Vientiane. (People's Daily Online/Xu Zheng)

Uzinduzi wa kampeni ya mahojiano ya pamoja kuhusu ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kati ya Gazeti la People's Daily la China na vyombo vya habari vya Laos umefanyika katika mji mkuu wa Laos, Vientiane, Jumanne wiki hii Juni 6.

Hii ni mara ya kwanza kwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali za China na Laos kuzindua kampeni ya pamoja ya mahojiano kuhusu ushirikiano wa BRI.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Vanxay Tavinyan, Naibu Mkuu wa Bodi ya Uenezi na Mafunzo ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi cha Laos na mhariri mkuu wa Gazeti la Laos Pasaxon, Phosy Keomanyvong, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Utalii ya Laos; Savankhone Razmountry, Rais wa Shirikiso la Waandishi wa Habari wa Laos; wawakilishi kutoka ubalozi wa China nchini Laos, na mashirika husika; na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na People's Daily, Pasaxon, Vientiane Times, Shirika la Habari la Laos na Televisheni ya Taifa ya Laos.

Katika hotuba yake Tavinyan amesema ushirikiano wa BRI umeleta fursa kubwa za maendeleo kwa nchi nyingi duniani, jambo ambalo si tu kwamba limeimarisha ushirikiano kati ya China na nchi shiriki na kuhimiza ushirikiano wa amani na maendeleo ya pamoja ya nchi mbalimbali, bali pia kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa binadamu.

“Chini ya mfumo wa BRI, Laos na China zimeimarisha ujenzi wa miundombinu,” ameongeza.

Kwa upande wake KaTavinyan amebainisha kuwa kuanza kufanya kazi kwa reli ya China-Laos na sehemu ya Vientiane-Vangvieng ya barabara kuu ya China-Laos kumeifanya Laos kutoka kuwa nchi isiyo na bahari hadi kuwa kitovu kilichounganishwa kwa nchi kavu, jambo ambalo limetoa fursa kubwa za ajira kwa watu wa Laos na kuongeza uchumi na maendeleo ya kanda.

Amesema gazeti la Pasaxon, kama kawaida, litaendelea kuandika na kuchapisha habari na makala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa BRI na mafanikio yake.

Baada ya uzinduzi huo, waandishi wa habari wa gazeti la People's Daily na wa vyombo vya habari vya Laos walifanya mahojiano kuhusu miradi muhimu iliyofanywa kwa pamoja kati ya China na Laos, kama vile Reli ya China-Laos na Eneo la Maendeleo la Vientiane Saysettha.

Mwaka huu inatimia miaka 10 tangu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lilipopendekezwa na China. Chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa China na Laos, nchi hizo mbili zimeendelea kuimarisha ushirikiano na kupata matokeo yenye manufaa katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Laos.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha