Kijiji cha Katikati mwa China chavuna Ngano kutwa kucha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2023
Kijiji cha Katikati mwa China chavuna Ngano kutwa kucha
Usiku wa tarehe 7, Juni, mashine ya kuvunia ikivuna ngano kwa dharura kwenye mashamba ya Kijiji cha Yuanying. (Picha ilipigwa na droni)

Kijiji cha Yuanying kiko kwenye Wilaya ya Huaxian ya Mji wa Anyang wa Mkoa wa Henan, ambayo inasifiwa kuwa “wilaya ya kwanza ya kilimo cha ngano nchini China”. Usiku wa terehe 7, Juni, mashine za kuvuna ngano zinapiga makelele mashambani, ambapo katibu wa kamati ya Chama ya kijiji hicho Wu Dongxing alijulisha kuwa, mashine hizi nne zitamaliza kazi ya mwisho ya kuvuna kwa dharura ngano kwenye mashamba ya hekta 20.

Asubuhi mapema ya terehe 8, mhusika wa kituo cha kukusanya nafaka cha Kijiji cha Yuanying Zhang Shouzhong alihangaika na kuandikisha kiasi cha ngano. “Leo tumevuna ngano zaidi ya kilogramu laki moja” alisema.

Katika majira ya joto ya mwaka huu, mvua mfululizo ilinyesha katika Mkoa wa Henan, ambao mazao yake ya ngano huchukua robo ya mazao ya jumla wa China. Shughuli mbalimbali za kuvuna ngano kwa dharura zilifanyika mashambani. Inafahamika kuwa, hadi saa 11 mchana tarehe 8, Juni, mkoa wa Henan umevuna ngano kwenye mashamba ya hekta 518.6, ambayo yanachukua asilimia 91 ya maeneo yote ya kupanda ngano katika mkoa huo.

(Picha zilipigwa na Zhang Haoran/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha