Ubalozi wa Jamhuri ya Honduras wafunguliwa rasmi mjini Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2023
Ubalozi wa Jamhuri ya Honduras wafunguliwa rasmi mjini Beijing, China
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akishiriki hafla ya kufunguliwa kwa ubalozi wa Jamhuri ya Honduras pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Enrique Reina anayezuru Beijing, China, Juni 11, 2023. (Xinhua/Li Tao)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje Qin Gang amehudhuria ameshiriki kwenye hafla ya kufunguliwa kwa ubalozi wa Jamhuri ya Honduras mjini Beijing pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Honduras Enrique Reina anayezuru China Jumapili.

Akitoa pongezi za dhati kwa kufunguliwa kwa ubalozi wa Honduras mjini Beijing, Qin amesema kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kwa msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja kumefungua zama mpya za uhusiano kati ya China na Honduras.

Akibainisha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeanza kwa nguvu katika miezi miwili iliyopita, Qin amesema maendeleo ya kasi ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili yamethibitisha kikamilifu kwamba ufuataji wa kanuni ya kuwepo kwa China moja unatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, unaakisi mwelekeo wa nyakati, matamanio ya watu, na hutumikia masilahi ya kimsingi ya nchi na watu wa pande hizo mbili.

Akirejea kauli ya Qin, Reina amesema kuwa kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na China kunafungua zama mpya katika uhusiano wa Honduras na dunia na kunatoa fursa kwa Honduras kuwa nchi kubwa na yenye ustawi.

Amesema, upande wa Honduras utatii kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inaamini kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kuimarika na kutoa matokeo yenye tija kwa manufaa ya watu wa pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha