Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya Ikolojia ya China Qinghai Yafunguliwa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 19, 2023
Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya Ikolojia ya China Qinghai Yafunguliwa
Mfanyabiashara akijulisha bidhaa za kiikolojia kwa wageni. Picha imepigwa na Gan Haiqiong/People’s Daily Online

Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya Ikolojia ya China Qinghai yamefunguliwa katika Mkoa wa Qinghai, China kuanzia Alhamisi, Tarehe 15, Juni.

Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Biashara ya China, Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya Asili ya China, Kamati ya Uhimizaji wa Biashara ya Kimataifa ya China, na serikali ya Mkoa wa Qinghai, maonesho hayo yamefuatiliwa na kuungwa mkono na wadau mbalimbali ndani na nje ya China, na kuhimiza mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu wa ikolojia na ushirikiano wa kimataifa. Washiriki kutoka mashirika 12 ya Kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Biashara Duniani (WTO), wanadiplomasia kutoka ubalozi wa nchi 37 nchini China na wajumbe wa mashirikisho ya biashara, kampuni na vyombo vya habari walikwenda Qinghai na kushiriki kwenye maonesho hayo.

Aidha, Maonesho ya Kimataifa ya Mazulia ya Kitibeti ya Qinghai 2023 yameanyika yakiwa ni maonesho madogo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Ikolojia ya China Qinghai. Maonesho hayo ya mazulia yamejulisha kwa pande zote utamaduni wa mazulia duniani, na kuonesha mazulia mengi bora ya ndani na nje pamoja na mazulia mazuri ya kitibeti. Mwaka huu ni mwaka wa 20 wa kufanyika kwa mfululizo kwa maonesho hayo ya blanketi za kitibeti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha