Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China waanza Mkutano wake Mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2023
Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China waanza Mkutano wake Mkuu
Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali, ikiwa ni pamoja na Xi Jinping, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi, wakihudhuria ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 19 wa Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China (CYLC) ili kutoa pongezi zao mjini Beijing, China, Juni 19, 2023. CYLC imeitisha mkutano wake mkuu wa 19 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing siku ya Jumatatu. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING - Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China umeanza Mkutano wake Mkuu wa 19 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing siku ya Jumatatu.

Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali, wakiwemo Xi Jinping, Zhao Leji, Wang Huning, Ding Xuexiang na Li Xi walihudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano huo kutoa pongezi zao. Cai Qi alitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), pamoja na viongozi wengine walikaribishwa kwa makofi ya shangwe walipofika ukumbini kabla ya ufunguzi wa mkutano.

Kwa niaba ya zaidi ya wanachama milioni 73 wa Umoja wa Vijana, karibu wajumbe 1,500 kutoka kote nchini China wamehudhuria mkutano huo.

Katika hotuba yake, Cai amesema chini ya uongozi madhubuti wa Kamati Kuu ya CPC, Umoja wa Vijana umechukua Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya kama mwongozo wake tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Umoja wa Vijana. Amesema, Umoja wa Vijana umeongeza uelewa wake wa kisiasa, kuongeza hali yake ya utangulizi na uwezo wa kuwakilisha watu, na kuimarisha uongozi, oganaizesheni, na huduma zake.

“Kutimiza lengo la pili la Miaka 100 la China la kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika pande zote na kuendeleza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China katika sekta zote kupitia njia ya maendeleo ya kisasa ya China ni kazi kuu ya CPC na pia ni mada ya harakati za vijana wa China na kazi ya vijana katika zama mpya,” Cai amesema.

Amewataka vijana nchini China kujitahidi kuwa vijana wa kizazi kipya cha zama mpya wenye matumaini, ujasiri na moyo wa kujitolea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha