Mji wa Qufu katika Mkoa wa Shandong, China mahali alipozaliwa Confucius, mwanafalsafa wa kale wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2023
Mji wa Qufu katika Mkoa wa Shandong, China mahali alipozaliwa Confucius, mwanafalsafa wa kale wa China
Picha hii iliyopigwa Juni 8, 2023 ikionyesha Hekalu la Confucius, jumba la kifahari la ukoo wa Kong na mandhari ya mji yanayozunguka maeneo hayo katika Mji wa Qufu, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Guo Xulei)

Mji wa Qufu, ulioko Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, ndipo alipozaliwa Confucius, mwanafalsafa wa kale wa China.

Kaburi la Confucius, Hekalu la Confucius na jumba la kifahari la ukoo wa Kong huko Qufu ni miongoni mwa maeneo maalum ya watu kuwakumbuka wanafalsafa wa kale wa China na maeneo muhimu kwa ajili ya ziara ya elimu na utafiti kuhusu utamaduni mzuri wa jadi wa China.

Zaidi ya hayo, Taasisi ya Utafiti wa Confucius ya China, Ardhi takatifu ya Nishan na Jumba la Makumbusho la Confucius huko Qufu, pia yanakuza utafiti na urithi wa Fikra za wasomi wa Confucius. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha