

Lugha Nyingine
Treni ya subway inayounganisha Miji ya Suzhou na Shanghai nchini China yafunguliwa kwa umma
![]() |
Abiria wakionekana kwenye Stesheni ya Huaqiao ya Laini 11 ya Subway ya Suzhou katika Mji wa Kunshan, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Juni 24, 2023. (Xinhua/Li Bo) |
NANJING – Siku ya Jumamosi reli ya Laini 11 ya mfumo wa Subway wa Suzhou ilianza kufanya kazi rasmi, mfumo huo ukiunganisha Mji wa Suzhou, ambao ni mchangiaji mkuu wa Pato la Kiuchumi (GDP) katika Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China na Shanghai, mji mwingine wenye mchango mkubwa kiuchumi katika eneo hilo.
Hii ni mara ya kwanza kwa miji mikubwa ya kiini katika eneo la Delta ya Mto Changjiang kuunganisha mifumo yao ya sabwe inayovuka mipaka ya mambo ya utawala ya ngazi tofauti ya kimkoa na vizuizi vya kijiografia katika maeneo tofauti.
Kwa mujibu wa usanifu wa mfumo wa sabwe, Laini hiyo mpya ya 11 iliyozinduliwa ya subway ya Suzhou pia ni sehemu ya Laini ya 11 ya subway ya Shanghai.
Njia hiyo ya sabwe inayovuka mikoa inaweza kupunguza muda wa kusafiri kati ya Mji wa Suzhou na Shanghai hadi takriban saa mbili. Njia hiyo ilipangwa kujenga mapema kama muongo mmoja uliopita.
"Kwa kweli, Laini ya 11 ni njia ya sita ya subway ya Suzhou na ilipewa jina mapema wakati huo, kuonyesha nia ya mji huo kuunganishwa vyema katika eneo la Delta ya Mto Yangtze," amesema Lu Wenxue, meneja mkuu wa Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la Suzhou.
Abiria sasa wanaweza kubadili laini za sabwe za miji hiyo miwili kwenye Stesheni ya Kunshan Huaqiao katika Mji wa Kunshan wa Jiangsu. Hasa, Kunshan imeorodheshwa ya kwanza kwa miaka 18 mfululizo kati ya miji 100 ya kiwilaya yenye nguvu zaidi nchini China.
Kuzinduliwa kwa njia hiyo ya sabwe kati ya miji pia kunafungua njia kwa maendeleo zaidi ya ushirikiano wa Suzhou na Shanghai. Kwa sasa, kampuni zilizo kwenye orodha ya kampuni bora 500 duniani zimeanzisha viwanda vyao huko Shanghai huku zikiweka makao makuu yao mjini Suzhou.
Katika siku zijazo, Laini ya 3 ya subway ya Suzhou pia itarefushwa hadi kufika Mji wa Wuxi mkoani Jiangsu, kuruhusu abiria wanaotumia sabwe mjini Shanghai kufikia miji zaidi magharibi mwake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma