

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akutana na mwenzake wa Sri Lanka Ali Sabry
![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akikutana na Ali Sabry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, mjini Beijing, China, Juni 25, 2023. (Xinhua/Zhang Ling) |
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amekutana na Ali Sabry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, mjini Beijing siku ya Jumapili.
Katika mazungumzo kati ya wanadiplomasia hao wawili, Qin amesema China na Sri Lanka zimekuwa zikiheshimiana na kusaidiana tangu zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, na kuweka mfano mzuri wa mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi zenye ukubwa tofauti.
Amezitaka pande hizo mbili kutekeleza kikamilifu makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa nchi zote mbili, kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya kati na ya juu kati ya watu, na kuhimiza ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Qin ameongeza kuwa, China itaendelea kutoa usaidizi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Sri Lanka na kuboresha maisha ya watu kadiri iwezavyo.
Sabry ameipongeza China kama rafiki mkubwa na mshirika muhimu katika maendeleo ya Sri Lanka, Sabry amesema Sri Lanka inathamini msaada usio wa ubinafsi unaotolewa na serikali na watu wa China kwa uhuru wa nchi hiyo na maendeleo yake kiuchumi, na ameishukuru China kwa uungaji wake mkono muhimu kwa Sri Lanka katika kushughulikia suala la deni na kushinda matatizo ya muda mfupi.
“Sri Lanka itaendelea kushikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, kuhakikisha ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kufanya kazi kwa uratibu wa karibu na China katika majukwaa ya uhusiano wa pande nyingi, na kuhimiza maendeleo zaidi ya uhusiano wa nchi hizo mbili,” Sabry ameongeza.
Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa na ya kikanda yanayofuatiliwa nazo pamoja. Qin amesema katika kukabiliana na hali ngumu na yenye utatanishi , China itashirikiana na nchi nyingine kulinda amani, utulivu na ustawi wa kikanda na Dunia na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma