Hafla ya kuhesabu siku 30 kabla ya Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU kuanza yafanyika Chengdu (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2023
Hafla ya kuhesabu siku 30 kabla ya Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU kuanza yafanyika Chengdu
Mkimbiza Mwenge Feng Zhe akionekana kwenye mbio za mwenge wa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 katika Chuo Kikuu cha Yibin huko Yibin, Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 28, 2023. (Xinhua/Wang Xi)

CHENGDU - Wakati inabakia siku 30 kabla ya kufanyika kwa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021, shughuli mfululizo zenye msisimko mkubwa za kusherehekea zimepamba mji mwenyeji wa Chengdu, Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China siku ya Jumatano.

Michezo hiyo iliahirishwa mara mbili kwa sababu kadhaa, huku janga la UVIKO-19 likiwa kikwazo kikubwa ambacho kilileta changamoto kubwa kwa kazi ya maandalizi.

Hata hivyo, katika muda wa miaka mitatu iliyopita, Chengdu imesimamia kwa mafanikio ujenzi, ukarabati, na upanuzi wa viwanja na kumbi za mazoezi 49. Miundoimbinu hiyo inajivunia vifaa vya hali ya juu na programu ya huduma, inayozingatia viwango vya mashindano ya kimataifa.

Kuanzia Aprili, shughuli kumi na nane za majaribio zimehitimishwa, zikihusisha washiriki 5,825 kutoka timu 367.

Alan Shaw, mtaalam kutoka kamati ya maandalizi ya michezo hiyo, ameonyesha imani yake juu ya kufanyika kwa mafanikio kwa michezo hiyo baada ya kuhitimisha shughuli ya majaribio ya mchezo wa kunyumbua viungo vya mwili kwa kufuata mdundo kwenye ukumbi wa mchezo huo wa Chuo Kikuu cha Michezo cha Chengdu.

Mwezi Mei, Gianni Merlo, Mkuu wa Shirikisho la Waandishi wa Habari za Michezo la Kimataifa (AIPS), pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, walihudhuria Mkutano wa Dunia wa Vyombo vya Habari uliofanyika Chengdu. Merlo alipongeza viwanja vya mji huo kuwa vyenye ubora wa kiwango cha Olimpiki na alionyesha kustaajabishwa na mazingira ya mji huo.

Tarehe 10, Juni, mbio za mwenge kwa ajili ya michezo hiyo zilianza kwa hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Peking, mjini Beijing. Mwenge huo, uliopewa jina la "Rong Huo", umekimbizwa katika miji kadhaa ya China, ikiwa ni pamoja na Beijing, Harbin, Shenzhen, Chongqing na Yibin.

Chengdu utakuwa mji wa tatu katika China Bara kuandaa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya majira ya joto, baada ya Beijing kuandaa Mwaka 2001 na Shenzhen Mwaka 2011.

Michezo hiyo ya Chengdu 2021 itahusisha shughuli 269 katika michezo 18.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha