Treni ya kitalii ya "Dayun" yaanza kufanya kazi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2023
Treni ya kitalii ya
Mchezaji akifanya maonesho ya opera ya Sichuan ya kubadilisha uso kwenye treni ya C3346, tarehe 29, Juni.

Saa nne na dakika nne mnamo tarehe 29 Juni mwaka 2023, Treni ya C3346, ambayo ni treni ya kitalii ya "Dayun" inayosafiri miji inayozunguka Chengdu, iliondoka kutoka Stesheni ya Reli ya Mashariki ya Chengdu na kuelekea Stesheni ya Reli ya Ya'an, ikiashiria kuwa treni ya kitalii ya "Dayun" ilizinduliwa rasmi katika mji wa Chengdu, mkoani Sichuan. Kwa mujibu wa idara ya utamaduni, redio, televisheni na utalii ya Chengdu, Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU itafanyika huko Chengdu mnamo Julai mwaka huu. Kuzinduliwa kwa treni ya kitalii ya "Dayun" kumechanganya utamaduni wa michezo na vipengele vipekee vya utamaduni wa Sichuan kama vile utamaduni wa Bashu na utamaduni wa panda, ili abiria waweze kuhisi hali ya michezo huo huku wakihisi haiba ya utamaduni wa Sichuan wakiwa safarini. (Picha na Hu Zhiqiang/Tovuti ya Gazeti la Umma)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha