Maofisa na Wataalam wa Ethiopia wapongeza Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kuwa ni ushirikiano wa kunufaishana (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2023
Maofisa na Wataalam wa Ethiopia wapongeza Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kuwa ni ushirikiano wa kunufaishana
Waziri wa Usafirishaji na Uchukuzi wa Ethiopia Alemu Sime akiwa kwenye treni inayotoa huduma kwenye Reli ya Ethiopia-Djibouti mjini Addis Ababa, Ethiopia, Juni 30, 2023. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Wataalamu na watunga sera wa Ethiopia wamesifu Pendekezo la China la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) siku ya Ijumaa wakisema kuwa ni jukwaa la ushirikiano wa kunufaishana katika kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Ethiopia na kwingineko.

Pongezi hizo zimetolewa kwenye mkutano wa ngazi ya juu wenye mada "China-Ethiopia zinajenga Ukanda Mmoja na Njia Moja." Mkutano wa majadiliano uliowakutanisha pamoja maofisa wakuu wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China nchini Ethiopia, maafisa kutoka Kampuni ya Reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti (EDR), wakuu wa taasisi za wataalam na watafiti, pamoja na viongozi wa vyombo vya habari, miongoni mwa wengine.

Waziri wa Usafirishaji na Uchukuzi wa Ethiopia, Alemu Sime amesema kwenye mkutano huo kuwa ikiwa ni mshirika muhimu wa China katika ujenzi wa BRI, Ethiopia imeshirikiana na China kwa karibu katika nyanja ya usafirishaji, na nchi hizo mbili zimesaidiana kwa manufaa ya kila mmoja, na kuonyesha uwezo mkubwa kwa ajili ya maendeleo.

"Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limekuwa jukwaa la ushirikiano wa kimataifa lililo wazi na jumuishi, lenye kunufaishana na faida kwa pande zote zinazoshiriki. Tunaishukuru serikali ya China kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya usafirishaji nchini Ethiopia," amesema waziri huyo.

Amesema reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti iliyojengwa na China yenye urefu wa kilomita 752.7, ambayo pia inajulikana kwa jina la reli ya Addis Ababa-Djibouti, kama kielelezo mojawapo cha BRI, imeleta msukumo muhimu kwa matarajio ya maendeleo ya Ethiopia.

Abdi Zenebe, afisa mkuu mtendaji wa EDR, amezungumzia mchango wenye manufaa wa BRI katika kuimarisha maendeleo ya kimataifa. "Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja linawakilisha maono ya ajabu, ambayo yanavuka mipaka, kuunganisha mabara, na kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea," amesema.

Kama "mfano mwanzilishi wa ushirikiano kati ya China na Afrika na kinara wa Afrika katika ujenzi wa BRI" Amesisitiza zaidi kujitolea na utayari wa serikali ya China kuunga mkono matarajio ya Ethiopia ya kujiendeleza kupitia BRI na mipango mingine ya maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha