

Lugha Nyingine
Kubadilisha kijiji tupu kilichotelekezwa kuwa kivutio kizuri cha watalii (2)
![]() |
Watalii wakipiga picha kwenye mkahawa katika Kijiji cha Hengshanwu huko Anji, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Juni 5, 2023. (Xinhua/Cai Yang) |
HANGZHOU - Karibu miaka 20 iliyopita, msanifu majengo Chen Gu alirudi makazi yake alikozaliwa kujiandaa kuanzisha biashara, lakini badala yake akachukua mradi wa kukarabati kijiji tupu kinachosimamiwa na Kijiji cha Hengshanwu huko Anji, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China.
Hengshanwu wakati huo kilikuwa kijiji maskini kilicho na mazingira mabaya kutokana na shughuli za uchimbaji madini. Uoto wa asili wa eneo hilo uliharibiwa na mitaro ya maji taka ilitoa harufu mbaya. Kwa hiyo, wenyeji wengi walihama.
"Hapo awali, ilinibidi kubeba baiskeli yangu begani ili kutembea kurudi kijijini wakati mvua ikinyesha kwa sababu ya barabara za udongo zenye matope hapa," Cai Mingfu, Mkuu wa tawi la Kijiji cha Hengshanwu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
Kijiji hicho kilishuhudia mabadiliko Mwaka 2003, wakati Mkoa wa Zhejiang ulipozindua Mpango wa Ustawishaji wa Kijani Vijijini, ambao ulihusisha kukarabati takriban vijiji 10,000 vilivyojumuishwa na kubadilisha takriban vijiji 1,000 kati yake kuwa mifano ya ustawi katika mambo yote.
Kutokana na mpango huo, kijiji hicho kilianza kampeni ya ukarabati na ujenzi vijijini, na kufanya maboresho makubwa katika kuzishindilia barabara zake, ukusanyaji wa taka na uchimbaji wa mitaro yake katika miaka iliyofuata.
Kikiwa na sura mpya kabisa, Kijiji cha Hengshanwu kilianza kuhimiza uchumi wake wa utalii kwa nguvu juu ya msingi wa rasilimali zake bora za asili. Serikali za mtaa zilimwalika Chen mzaliwa wa Anji kusaidia kujenga kijiji ambacho hapo awali kilikuwa tupu kwa kutelekezwa na kukibadili kuwa jumuiya ya watalii.
Wenyeji wanaweza kukodisha nyumba zao kwa timu ya usimamizi wa kitaalamu ya Chen, au wanaweza kuendesha hoteli zao wenyewe. "Hatutaki kuwafukuza watu, bali kufanya kazi nzuri katika sekta ya utalii wa kitamaduni vijijini na kufikia ustawi wa pamoja," Chen amesema.
Mwaka 2022, Xiaoyin ilikuwa sehemu maarufu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, ikipokea wageni zaidi ya 350,000, na kuzalisha mapato ya kila mwaka ya zaidi ya yuan milioni 67 (sawa na dola za Kimarekani milioni 9.29). Wastani wa mauzo yake ya kila siku yalikuwa zaidi ya yuan 40,000 wakati wa likizo ya Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma