Rais Xi Jinping ahudhuria mkutano wa SCO, atoa wito wa mshikamano na uratibu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2023
Rais Xi Jinping ahudhuria mkutano wa SCO, atoa wito wa mshikamano na uratibu
Rais Xi Jinping wa China akihutubia mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa njia ya video kutoka Beijing, China, Julai 4, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesema Jumanne kwamba Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) lazima ijitokeze kutii wito wa nyakati, kutilia maanani dhamira ya kuanzishwa kwake, na kushikilia mshikamano na uratibu ili kuleta uhakika zaidi na nishati chanya kwa amani na maendeleo ya Dunia.

Rais Xi ameyasema hayo alipohutubia mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa njia ya video kutoka Beijing.

Amesema miaka kumi iliyopita, kwa kutilia maanani mabadiliko ya Dunia, nyakati na historia, alitoa pendekezo kwamba wanadamu, wanaoishi katika kijiji kimoja cha Dunia, wanazidi kuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ambayo kila maslahi ya mtu mmoja yanahusiana kwa karibu.

Kuanzia wakati huo, dhana ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja imepata kutambuliwa na kuungwa mkono kwa pande zote kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, na imekuwa ikibadilika kutoka kuwa wazo hadi vitendo na matarajio hadi hali halisi.

Amesema, nchi wanachama zimeendeleza moyo wa ujirani mwema, na kutetea usawa, kufundishana , kuwa na mazungumzo na ujumuishaji kati ya ustaarabu mbalimbali, na kutoa wito wa kuishi pamoja kwa amani na maendeleo yenye usawa ya ustaarabu tofauti.

Viongozi waliohudhuria mkutano huo wamepongeza mafanikio dhahiri ya maendeleo ya SCO , kuikaribisha Iran kuwa nchi mwanachama rasmi na wameeleza matumaini yao kuwa Belarus itakamilisha taratibu za kujiunga na SCO haraka iwezekanavyo.

Wameeleza kuwa SCO imekuwa ikikua huku ikiwa na ushawishi mkubwa wa kimataifa, ikitoa mchango muhimu katika kuimarisha ujirani mwema na urafiki, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi wanachama, kuhimiza amani na utulivu wa kudumu katika kanda na Dunia, na kuhimiza maendeleo endelevu. Wamesema jumuiya hiyo imekuwa kielelezo cha kuaminiana, kufanya mazungumzo kwa usawa na ushirikiano wa kunufaishana.

Pia wametaka kufanyika kwa juhudi za pamoja za kupambana na nguvu za ugaidi, vikundi vinavyotaka kujitenga na vyenye misimamo mikali na kudumisha ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kuunga mkono Umoja wa Mataifa kufanya kazi ya uongozi na kuimarisha usimamizi wa Dunia.

Kwenye mkutano huo, imeamuliwa kwamba Kazakhstan itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa SCO Mwaka 2023-2024.

Mkutano huo wa mwaka huu umeendeshwa na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ukiwakutanisha Rais Xi na viongozi kutoka nchi wanachama za Kazakhstan, Kyrgyzstan, Pakistan, Russia, Tajikistan na Uzbekistan pamoja na nchi washiriki waangalizi za Belarus, Iran, na Mongolia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha