

Lugha Nyingine
China na Umoja wa Ulaya zafanya mazungumzo kuhusu mazingira na tabianchi (2)
![]() |
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang na Makamu Mkuu Mtendaji wa Kamisheni ya Ulaya Frans Timmermans wakifanya mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya Mazingira na Tabianchi kati ya China na Umoja wa Ulaya, mjini Beijing, China, Julai 4, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei) |
BEIJING - Mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya Mazingira na Tabianchi kati ya China na Umoja wa Ulaya (EU) yamefanyika Jumanne mjini Beijing, na pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano na kubeba wajibu wa kiuongozi katika usimamizi wa kimataifa wa mazingira na tabianchi.
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang na Makamu Mkuu Mtendaji wa Kamisheni ya Ulaya Frans Timmermans wamefanya mazungumzo.
Ding, amesema pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa pande zote mbili, kuhimiza ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya kuhusu mazingira na tabianchi ili kufikia mafanikio zaidi, na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo endelevu ya kimataifa.
Huku akitoa wito kwa pande hizo mbili kuendeleza kwa pamoja mchakato wa pande nyingi kuhusu mazingira na tabianchi na utekelezaji wa matokeo ya COP15, Ding amesema, China inatilia maanani sana ulinzi wa ikolojia na mazingira na mabadiliko ya tabianchi, inahimiza bila kuyumba maendeleo ya kijani na yanayotoa kaboni chache, na imeanzisha hatua mbalimbali za kuhakikisha inafikia malengo ya kilele cha utoaji wa kaboni na kusawazisha kaboni kwa wakati uliopangwa.
"China iko tayari kushirikiana na Umoja wa Ulaya kutumia vyema mazungumzo kuhusu mazingira na tabianchi, kujenga zaidi maelewano, kuaminiana, kuimarisha na kupanua ushirikiano, na kufungua nafasi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya" Ding amesema, na kuongeza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kutumia uwezo wa ushirikiano katika nishati mbadala, teknolojia zinazosaidia mazingira na kutoa kaboni chache, masoko ya kaboni, mwitikio wa mabadiliko ya tabianchi, na ulinzi wa ikolojia na mazingira.
Kwa upande wake Timmermans amesema kuwa EU na China zimekuwa na wajibu muhimu katika mwitikio wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi. Amesema EU iko tayari kuimarisha ushirikiano na China katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa mzunguko, ulinzi wa viumbe anuai na nyanja nyingine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma