

Lugha Nyingine
IAEA yakanusha kuidhinisha uamuzi wa serikali ya Japan kutupa maji taka ya nyuklia baharini (2)
![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi (kushoto) akitoa ripoti ya utathmini wa usalama kuhusu mpango wa Japan wa kutupa maji taka ya nyuklia baharini kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima Daiichi kilichoacha kutumika kwa Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida huko Tokyo, Japan, Julai 4, 2023. (Xinhua/Zhang Xiaoyu) |
TOKYO – Ripoti iliyowasilishwa Jumanne na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi inasema kuwa, Shirika la IAEA haliidhinishi uamuzi wa serikali ya Japan kwa ripoti yake ya utathmini wa usalama juu ya mpango wa Japan wa kutupa maji taka ya nyuklia baharini kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima Daiichi.
"Ninapenda kusisitiza kwamba kutupwa baharini kwa maji taka ya nyuklia yaliyosafishwa ambayo yalihifadhiwa katika Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima Daiichi ni uamuzi wa Serikali ya Japan na kwamba ripoti hii siyo pendekezo au uidhinishaji wa sera hiyo," Grossi ameeleza katika dibaji ya ripoti hiyo, ambayo ameiwasilisha ana kwa ana hapa Jumanne kwa Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida.
"Maoni yaliyotolewa hapa si lazima yaakisi yale ya Nchi Wanachama wa IAEA," imesema ripoti hiyo, huku ikibainisha kwamba "si IAEA wala Nchi Wanachama wake zinazochukua jukumu lolote kwa matokeo ambayo yanaweza kutokea kutokana na matumizi yake."
Serikali ya Japan imekuwa ikishinikiza kuanza kutupa maji taka hayo baharini majira haya ya joto, jambo ambalo limezua upinzani mkali na mashaka kutoka kwa makundi ya wavuvi wenyeji, nchi jirani, maeneo ya pwani ya Bahari ya Pasifiki, nchi za visiwa vya Bahari ya Pasifiki Kusini, na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.
Pia siku ya Jumanne, vyombo viwili vya habari vya Korea Kusini vilisema kwamba Japan imesaini "mkataba mweusi" na IAEA "kuondoa" masuala nyeti yaliyotajwa katika ripoti yake ya mwisho, ikinukuu vyanzo vya habari visivyojulikana.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin Jumanne alisema kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kwamba China inaamini kwamba IAEA inapaswa kufikia hitimisho juu ya jambo hilo ambalo linawajibika na linaweza kukabiliana na mtihani wa historia na sayansi, na lazima lisiidhinishe makosa ya Japan katika kutupa maji taka ya nyuklia.
Kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan, Grossi ameanza ziara yake ya siku nne nchini Japan siku ya Jumanne, ikiwa ni pamoja na ziara ya kutembelea kituo cha nyuklia cha Fukushima Daiichi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma