

Lugha Nyingine
Ghana yafungua tena Eneo la Kumbukumbu ya Kwame Nkrumah ili kuimarisha utalii (3)
![]() |
Watalii wakitembelea Eneo Maalum la Kumbukumbu ya Kwame Nkrumah huko Accra, Mji Mkuu wa Ghana, Julai 4, 2023. (Picha na Seth/Xinhua) |
ACCRA - Ghana imefungua tena Eneo la Kumbukumbu ya Kwame Nkrumah siku ya Jumanne, eneo ambalo ni urithi mkubwa wa kitamaduni katika mji mkuu, Accra wa kumkumbuka rais wa kwanza wa nchi hiyo, kwa matumaini ya kukuza utalii.
Eneo hilo, lililofunguliwa kwa mara ya kwanza Mwaka 1992, limekamilisha ukarabati wake chini ya mradi wa miaka mitano wa serikali ya Ghana wa kuhimiza sekta ya utalii na ukarimu kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Sasa eneo hilo lililokarabatiwa lina maktaba ya rais, kituo cha mapokezi, ukumbi mdogo wa michezo na maonyesho, mgahawa, na mfumo wa malipo wa kidijitali.
Kwenye hafla ya ufunguzi tena wa eneo hilo, Rais wa Ghana Nana Addo Dankwa Akufo-Addo amesema serikali inapanga kulifanya eneo hilo kuwa moja ya vivutio bora vya utalii na urithi katika ukanda wa Afrika Magharibi.
"Eneo alilozikwa Kwame Nkrumah lazima liendane na hadhi yake ya kuwa mtu mashuhuri anayepinga ukoloni na ubaguzi wa rangi wa kizazi hiki na kwa mchango wake wa kipekee katika ukombozi wa Afrika kutoka kwa ukoloni na ubeberu," Rais Addo amesema.
Ameelezea matumaini yake kwamba eneo hilo, ambalo lilivutia watalii 90,000 kila mwaka kabla ya ukarabati, litaweza kuvutia watalii zaidi ya milioni moja kila mwaka baada ya ukarabati.
Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Pierre Laporte, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Ghana, Liberia na Sierra Leone, amesema Benki ya Dunia ina furaha kuunga mkono ukarabati huo na itaendelea kusaidia sekta ya utalii ya Ghana. "Kwame Nkrumah hadi leo anachukuliwa kuwa mmoja wa viongozi muhimu zaidi wa Karne ya 20."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma