Mji wa Beijing, China watoa tahadhari nyekundu ya joto kali (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2023
Mji wa Beijing, China watoa tahadhari nyekundu ya joto kali
Watu wakitembelea Mtaa wa Qianmen mjini Beijing, China, Julai 6, 2023. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING - Mji wa Beijing nchini China umetoa tahadhari nyekundu ya joto kali siku ya Alhamisi, ambayo ni ya juu zaidi katika mfumo wa tahadhari wenye kuwakilishwa kwa rangi tofauti, huku hali joto katika maeneo mengi ya mji huo ikikadiriwa kuongezeka na kufikia juu ya nyuzi joto 40.

Hii ni tahadhari ya pili nyekundu ya joto kali kutolewa na mji mkuu huo wa China katika majira haya ya joto.

Hali joto katika kituo cha hali ya hewa cha Nanjiao, Kusini mwa Beijing ilipanda hadi nyuzi joto 40.9 siku ya Jumatano, amesema He Na, mtabiri mkuu wa hali ya hewa wa Idara ya Uchunguzi wa Hali ya Hewa ya Beijing.

Kituo hicho kimerekodi siku 18 zenye hali joto inayofikia nyuzi joto 35 au zaidi, na siku nne zenye hali joto inayofikia nyuzi joto 40 au zaidi kati ya Juni na Julai 5, ambazo zote ni za kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa katika kipindi kama hicho tangu kituo hicho kilipoanzishwa Mwaka 1951.

Mji huo utaendelea kuwa katika hali joto ya juu kuanzia Alhamisi hadi leo Ijumaa, kwa mujibu wa utabiri.

Idara hiyo ya utabiri wa hali ya hewa ya Beijing imewashauri wakazi kupunguza shughuli za nje na kuchukua hatua zinazofaa ili kuzuia joto na kuchomwa na jua wakati wa kwenda nje.

Tangu Mwezi Juni, mikoa ya kaskazini na maeneo mengine ya China yamekumbwa na raundi tano za mawimbi ya joto, huku kiwango cha juu cha hali joto kila siku kikifikia nyuzi joto 35 au zaidi, na maeneo mengi katika eneo la Beijing-Tianjin-Hebei yamevunja rekodi za kihistoria.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha