Kukiwa na wasiwasi juu ya ripoti ya IAEA, umma ya Japan wapinga mpango wa kutupa maji taka ya nyuklia (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2023
Kukiwa na wasiwasi juu ya ripoti ya IAEA, umma ya Japan wapinga mpango wa kutupa maji taka ya nyuklia
Mwandamanaji akishiriki maandamano ya kupinga mpango wa Japan wa kutupa maji taka ya nyuklia mbele ya makao makuu ya Kampuni ya Umeme ya Tokyo (TEPCO), ambayo ni mwendeshaji wa Kituo cha Nishati ya Nyuklia cha Fukushima Daiichi kilichoharibika, huko Tokyo, Japan, Julai 5, 2023. (Xinhua/ Zhang Xiaoyu)

TAKYO - Takriban waandamanaji 100 wa Japan walikusanyika siku ya Jumatano kupinga mpango wa Japan wa kutupa maji taka ya nyuklia kwenye Bahari ya Pasifiki, wakielezea wasiwasi wao mkubwa juu ya ripoti ya mwisho ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).

Maandamano hayo yamefanyika Jumatano jioni mbele ya makao makuu ya Kampuni ya Umeme ya Tokyo (TEPCO), ambayo ni mwendeshaji wa Kiwanda cha Nyuklia cha Fukushima Daiichi kilichoharibika.

Waandamanaji kutoka vikundi kadhaa vya kiraia walionyesha mabango yaliyosomeka "Usimwage maji taka baharini" na "Usichafue bahari zetu."

"Kinachojulikana kuwa viwango vya usalama vya TEPCO vilikuwa na dosari kubwa," mwandamanaji mmoja mwenye jina la ubini la Yamazaki ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

"Kwa kuzingatia hatari vinavyoweza kusababisha katika siku zijazo, kutupa maji yenye mionzi ya nyuklia ndani ya bahari kwa kiasi kikubwa kama hicho hakuvumiliki " amesema.

Siku ya Jumanne, IAEA ilichapisha ripoti yake ya mwisho ya tathmini ya kina ya usalama juu ya mpango huo wa Japan wa kutupa maji taka hayo baharini, baada ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi kukabidhi ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida huko Tokyo wakati alipoanza ziara ya siku nne nchini Japan kwa mwaliko wa wizara ya mambo ya nje ya Japan.

Waandamanaji wametoa malalamiko juu ya ripoti hiyo, wakisema kwamba serikali ya Japan ilikuwa "isiyo na busara" kwa kuchukua ripoti ya IAEA kama "kibali cha kutupa maji taka baharini" kwa kupuuza kabisa upinzani kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo, sekta ya uvuvi, na nchi jirani.

Siku ya Jumanne alasiri, Grossi alisisitiza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari ya Japan huko Tokyo kufuatia utoaji wa ripoti ya IAEA kwamba chaguo la kutupa maji taka ya nyuklia baharini linapaswa kufanywa na serikali ya Japani.

“IAEA itakuwa na uwepo endelevu katika eneo la Kituo cha Nishati ya Nyuklia cha Fukushima Daiichi kukagua, kufuatilia na kutathmini shughuli za kutupa maji kwa miongo kadhaa ijayo,” Grossi alisema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha