Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China wakaribisha meli ya kwanza ya kitalii katika kipindi cha miaka mitatu (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2023
Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China wakaribisha meli ya kwanza ya kitalii katika kipindi cha miaka mitatu
Picha hii iliyopigwa Julai 8, 2023 ikionyesha meli ya kitalii ya Liberia, Dream, ikitia nanga kwenye bandari katika Mji wa Tianjin Kaskazini mwa China. (Xinhua)

TIANJIN - Meli ya kitalii iliyosajiliwa nchini Liberia imetia nanga kwenye bandari katika Manispaa ya Tianjin, Kaskazini mwa China siku ya Jumamosi, na kuwa meli ya kwanza ya kimataifa ya kitalii kupokelewa na bandari ya Tianjin katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Meli hiyo ya kitalii ya Dream, ina urefu wa mita 261 na upana wa mita 40, na uzito wake wa jumla ni tani 77,500. Inaweza kubeba abiria zaidi ya 2,000 na wahudumu zaidi ya 1,000.

Ili kuhakikisha meli hiyo inatia nanga na kupata huduma mbalimbali kwa ufanisi, mamlaka husika za Mji wa Tianjin zilisaidia wafanyakazi zaidi ya 60 wa China na wa kigeni kutimiza taratibu zote za kuingia bandarini kupitia mtandao.

Tianjin kwa muda mrefu imekuwa kitovu cha meli za kitalii katika eneo la Kaskazini mwa China. Kuja kwa meli hiyo ya kitalii ya Liberia kunaashiria kuwa sekta ya utalii ya mji huo umeanza kuimarika baada ya UVIKO-19.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha