

Lugha Nyingine
Kongamano la Kimataifa la Ikolojia la Guiyang 2023 lafungwa kwa mafanikio huko Guizhou, China (2)
![]() |
Wasanii wakiimba nyimbo za Kabila la Wadong kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Ikolojia la Guiyang 2023 huko Guiyang, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Julai 9, 2023. (Xinhua/Yang Wenbin) |
GUIYANG - Kongamano la Kimataifa la Ikolojia la Guiyang 2023 ambalo ni kongamano pekee la ngazi ya kitaifa nchini China lenye mada kuhusu ustaarabu wa ikolojia limehitimishwa Jumapili huko Guiyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China.
Kwenye kongamano hilo, Idara ya Hali ya Hewa ya China imetoa waraka juu ya mabadiliko ya tabianchi, ambao unachambua mwenendo mpya wa tabianchi nchini China, Asia na kote duniani.
Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) ulifanya hafla ya kutoa tuzo kwa hifadhi 13 za mazingira asilia nchini China ambazo ziliwekwa kwenye orodha yake ya kijani.
Kongamano hilo limevutia washiriki zaidi ya 3,200 kutoka nchi na maeneo 42, na makubaliano 14 yamefikiwa juu ya ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia na maendeleo ya kijani.
Kongamano hilo, ambalo limefanyika kwa siku mbili za Jumamosi na Jumapili, limelenga kutafuta maendeleo ya kisasa ya kuishi kwa maelewano na usawa kati ya binadamu na mazingira asilia, na kuhimiza maendeleo ya kijani na yanayotumia kaboni chache.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma