Mahojiano: NATO inatumia Ukraine kama kete ya kafara katika kuishinda Russia, asema mbunge wa Ujerumani (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2023
Mahojiano: NATO inatumia Ukraine kama kete ya kafara katika kuishinda Russia, asema mbunge wa Ujerumani
Watu wakishiriki maandamano dhidi ya Sweden kuandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa na jitihada za nchi hiyo kuwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) huko Stockholm, Sweden, Aprili 22, 2023. (Picha na Patrick Ekstrand/Xinhua)

BERLIN - Mbunge wa Ujerumani Sevim Dagdelen ameishutumu Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) kwa kupigana vita wakala dhidi ya Russia kwa kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

"Kama tutautazama mgogoro huu kama mchezo wa chess, basi NATO inatafuta kete ambazo zinaweza kutolewa kafara kama itahitajika, ili kupata nafasi nzuri," Dagdelen, ambaye ni mjumbe wa bunge la chini la Ujerumani, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Kwa kuwasilisha silaha na kupeleka washauri wa kijeshi wa NATO nchini Ukraine, NATO sasa inaendesha vita wakala dhidi ya Russia ili kuishinda nchi hiyo yenye nguvu za nyuklia kupitia mchanganyiko wa nguvu za kijeshi na vita vya kiuchumi vya pande zote, amesema Dagdelen, Mwenyekiti wa kundi la wabunge wa Die Linke (Chama cha Mrengo wa Kushoto) wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ujerumani, Bundestag.

Amesema kuwa NATO siyo jumuiya ya kujihami, ingawa huo ni msimamo wa mara kwa mara wa viongozi wa Magharibi.

"Wakati huo huo, jumuiya hiyo ya kijeshi inajitahidi kuandaa silaha na inazuia juhudi zote za mazungumzo kuhusu mgogoro wa Ukraine," amesema.

Mkutano wa kilele wa NATO, ambao unafanyika kwa siku mbili za Julai 11 hadi 12 mjini Vilnius, Lithuania, utaileta Ukraine karibu na jumuiya hiyo, alisema Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Jens Stoltenberg kabla ya mkutano huo.

"Majadiliano kabla ya mkutano wa kilele wa NATO yanatia wasiwasi sana," amesema, huku akiongeza kuwa mjadala unafanyika ndani ya NATO kuhusu kuipa Ukraine uanachama wa NATO au dhamana ya usalama ya NATO, hali ambayo itazusha vita kati ya NATO na Russia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha