Mazungumzo ya Vyama vya Siasa vya China na Nchi za Kiarabu yafanyika Kaskazini Magharibi mwa China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2023
Mazungumzo ya Vyama vya Siasa vya China na Nchi za Kiarabu yafanyika Kaskazini Magharibi mwa China
Wageni waalikwa wakihudhuria Mazungumzo ya nne ya Vyama vya Siasa vya China na Nchi za Kiarabu huko Yinchuan, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini-Magharibi mwa China, Julai 13, 2023. (Xinhua/Feng Kaihua)

YINCHUAN - Mazungumzo ya nne ya Vyama vya Siasa vya China na Nchi za Kiarabu yamefunguliwa Alhamisi huko Yinchuan, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini Magharibi mwa China.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Fatah, ametuma ujumbe wa maandishi kwa shughuli hiyo.

Yakiwa yameandaliwa na Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Chuo cha Kamati Kuu ya CPC, na Kamati ya CPC ya Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, wajumbe waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi wa kisiasa kutoka nchi 19 za Kiarabu na viongozi wa vyama vya kisiasa na mashirika 67.

Wakibainisha kuwa mazungumzo hayo ni jukwaa muhimu la mabadilishano na ushirikiano kati ya CPC na vyama vya siasa vya nchi za Kiarabu, wajumbe waliohudhuria mazungumzo hayo wameapa kuwezesha mabadilishano zaidi na kujifunza kutoka kila upande kati ya ustaarabu wa China na Nchi za Kiarabu, na kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Nchi za Kiarabu katika zama mpya.

Taarifa ya utekelezaji wa Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia imeidhinishwa kwenye mazungumzo hayo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha