

Lugha Nyingine
Kutembelea Kituo Kikuu cha Vyombo vya Habari cha Chengdu Universiade (5)
![]() |
Picha hii ikionesha sehemu ya mapokezi katika Kituo Kikuu cha Vyombo vya Habari cha Chengdu Universiade. (Picha na Fu Yuanyuan/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Michezo ya awamu ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 (ufupisho: Chengdu Universiade) itafanyika kuanzia Julai 28 hadi Agosti 8, 2023. Kama "nyumba ya waandishi wa habari" na "kitovu" cha upashanaji habari wakati wa michezo hiyo, Kituo Kikuu cha Vyombo vya Habari cha Chengdu Universiade kitawapa waandishi wa habari wa vyombo vya habari duniani zana na vifaa na huduma mbalimbali zinazohitajika wakati wa kuripoti michezo hiyo, zikiwa pamoja na ofisi, migahawa, vyombo vya usafiri, matibabu, burudani n.k.
Inafahamika kwamba eneo la jumla la ujenzi wa kituo kikuu cha vyombo vya habari ni takriban mita za mraba 45,000, ambapo kuna ghorofa moja ya chini ya ardhi na ghorofa tano juu ya ardhi, ndani yake ni pamoja na sehemu ya kazi ya vyombo vya habari, sehemu ya burudani, na sehemu ya shughuli za kitamaduni. Kwenye eneo la majengo hayo kuna zana na vifaa vingi vya kutosha, ambavyo vinaweza kuwapatia waandishi wa habari huduma mbalimbali.
Baada ya kufunguliwa rasmi, mfululizo wa shughuli zinazohusika na urithi usioshikika wa kitamaduni zitafanyika kwenye kituo kikuu cha vyombo vya habari, ili wanahabari wa vyombo vya habari kutoka duniani waweze kuelewa vyema zaidi mvuto wa utamaduni wa Bashu, kama vile Sanaa za hariri maalumu za Shu, Sanaa za utarizi wa hariri wa Shu, Sanaa za usukaji wa mianzi juu ya vyombo vya kaure, uchoraji picha kwa sukari, maonesho ya Chai ya Kung Fu, n.k.
Habari zinasema kuwa kituo kikuu cha habari kitaingia katika hali ya uendeshaji kwa saa 24 bila kusita kuanzia Julai 25 ambapo ripoti za mashindano ya michezo ya kusisimuka zitatolewa haraka iwezekanavyo kutoka kituo hicho na kuonesha uhondo wa michezo ya vijana kwa watu wa dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma