

Lugha Nyingine
Kijiji cha Michezo ya vyuo vikuu ya Chengdu chajaa teknolojia za kisasa
![]() |
Picha hii ikionesha basi inayojiendesha yenyewe huko kijiji cha FISU cha Chengdu. (Picha na Li Zheng/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Wakati Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu inakaribia, kazi ya kijiji cha FISU iko tayari kwa ujumla, na kijiji kitafunguliwa rasmi Julai 22 ili kukaribisha wanamichezo vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Kijiji cha FISU kiko kwenye Chuo Kikuu cha Chengdu, ambacho kinajengwa na kukarabatiwa kwa mujibu wa miundombinu na majengo ya Chuo Kikuu cha Chengdu. Eneo lake ni takriban mita za mraba 800,000, na eneo la jumla la majengo ni takriban mita za mraba 660,000. Hivyo kinaweza kupokea watu wapatao 11,000. Kuna majengo 10 ya bweni, mikahawa 2 ya wanamichezo katika kijiji hicho, pamoja na vifaa vya huduma kama vile kituo cha huduma na kituo cha matibabu.
Katika Kijiji hicho, vifaa vyenye teknolojia za juu zinaonekana kila mahali, kama vile basi inayojiendesha yenyewe, mfumo wa ukalimani mtandaoni unaoweza kutambua lugha 83, roboti inayoweza kutengeneza kahawa kwa kutumia sekunde 90 tu, na sanamu zinazotengenezwa kwa sekunde 3 mara baada ya kupigwa picha za 3D n.k. Vifaa hivyo vinahusisha mambo yote ya "maisha ya kijijini", kama vile chakula, malazi, usafiri na burudani na zinawafanya wanamichezo na wageni wahisi kwa kina haiba ya teknolojia ya Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani vya Chengdu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma