Wakandarasi wa China wakabiliana na joto ili kukamilisha sehemu ya mwisho ya mradi wa barabara kuu ya Algeria (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2023
Wakandarasi wa China wakabiliana na joto ili kukamilisha sehemu ya mwisho ya mradi wa barabara kuu ya Algeria
Picha hii iliyopigwa Agosti 18, 2022 ikionyesha wafanyakazi wa mradi kutoka CITIC Construction wakitumia mitambo ya ujenzi kuweka ukanda wa kuzuia moto ndani ya misitu katika Jimbo la El Tarf, Algeria. (Picha imetolewa na CITIC Construction/Xinhua)

ALGIERS - Licha ya jua kali Mwezi Julai, eneo la ujenzi wa Barabara Kuu ya Mashariki-Magharibi katika Jimbo la El Tarf, Mashariki mwa Algeria lina shughuli nyingi.

Wafanyakazi wa China na Algeria wanastahimili joto kali, wakiwa na shughuli nyingi za kutandaza lami na kufanya kazi ya mwisho kwa ajili ya uzinduzi wa barabara hiyo kwa matumizi ya umma.

"Sehemu hiyo ina umuhimu mkubwa kwa sababu uzinduzi wake unaashiria kukamilika kikamilifu kwa Barabara Kuu ya Mashariki-Magharibi yenye urefu wa kilomita 1,216, ambayo inaunganisha majimbo 17 ya Algeria na kuileta nchi hiyo karibu na nchi nyingine za Kiarabu," Djotni Benaissa, mkuu wa mradi huo kwenye Shirika la Taifa la Barabara Kuu la Algeria, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.

Barabara hiyo, inayovuka kutoka mpaka wa mashariki wa Algeria na Tunisia hadi mpaka wa magharibi na Morocco, inachukuliwa kuwa moja ya miradi muhimu zaidi ya nchi hiyo.

Novemba 2017, Algeria ilitia saini mkataba na Shirika la China International Trust and Investment (CITIC) ili kukamilisha sehemu ya mwisho yenye urefu wa kilomita 84 ya sehemu ya mashariki ya barabara kuu karibu na mpaka wa Tunisia, takriban miaka mitatu baada ya kutelekezwa na mkandarasi wa awali wa Japan kutokana na mgogoro wa malipo.

CITIC Construction, ambayo ilikuwa ikijenga sehemu nyingine za Barabara Kuu ya Mashariki-Magharibi, ilichaguliwa kuwa mkandarasi anayefuata wa mradi huo kutokana na kazi zake za awali za ajabu.

Mohamed Khaldi, mkurugenzi wa shirika hilo, ameipongeza CITIC Construction kwa "ufuataji wake wa sheria na kanuni za nchi hiyo na kanuni za kimataifa wakati wa kazi yake ya awali ya ujenzi wa barabara kuu," na kuongeza kuwa kampuni hiyo imetekeleza "teknolojia ya hali ya juu ili kuhakikisha viwango vya juu na ubora wa mradi".

"Wahandisi vijana wa Algeria, ambao wamepata uzoefu kupitia ushirikiano wa muda mrefu na wenzao wa China, wana ujuzi wa juu na wanawakilisha mustakabali wa sekta hiyo nchini Algeria," Mohamed Salah Kafi, mkuu wa ofisi ya kanda ya mashariki ya Shirika la Taifa la Barabara Kuu la Algeria.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha