

Lugha Nyingine
Habari picha ya mhudumu wa treni kwenye Reli kati ya China na Laos
Yi Bofeng anatoka Eneo la Mengla katika Mkoa wa Yunnan. Baada ya kuhitimu masomo ya lugha ya kiLao katika chuo cha ufundi cha Kunming Mwaka 2020, aliajiriwa kuwa mhudumu wa treni chini ya Shirika la Reli la China, Tawi la Kunming.
Reli ya China na Laos, mradi wa kihistoria wa ushirikiano wa hali ya juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, ilianza kufanya kazi Desemba 2021. Yi alikuwa ndani ya treni ya kwanza ya reli hiyo, akishuhudia wakati wa kihistoria wa uendeshaji wa reli hiyo.
Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,035 inaunganisha Mji wa Kunming nchini China na Vientiane nchini Laos. Reli hiyo imesafirisha zaidi ya abiria milioni 16.4 na mizigo yenye uzito wa zaidi ya tani milioni 21 hadi kufikia Juni 3 mwaka huu.
Reli hiyo ilianza huduma za usafirishaji wa abiria wa kuvuka mpaka Aprili 13 mwaka huu. Treni moja ya abiria inafanya safari za kila siku kutoka Kunming hadi Vientiane na nyingine inafanya safari kutokea Vientiane hadi Kunming. Tangu wakati huo, Yi ametoa huduma kwa zaidi ya safari 20 za kwenda na kurudi.
Kando ya njia hiyo ya reli kuna maeneo yenye rasilimali nyingi za utalii, rasilimali nyingi za spishi, na mkusanyiko mkubwa wa urithi wa asili na wa kitamaduni. Vijiji vilivyo chini ya Eneo la Mengla ambako familia ya Yi huishi hujivunia upandaji wa miti ya mpira na matunda. Kwa sababu vijiji hivyo viko karibu na reli, bidhaa kutoka vijiji hivyo zinaweza kufikia sokoni haraka ili wanakijiji wafurahie faida zinazoletwa na reli hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma